PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

UTAJUAJE KAMA SIKU YAKO YA KIFO IMEFIKA?


Si rahisi kujua siku yako ya kifo, lakini kuna watu hupata bahati ya kujua muda umefika. Hapa ni baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia kujua kuwa saa yako ya kifo imewadia…..
UTAJUA KUWA MUDA UMEFIKA..pale ambapo majambazi wenye silaha wameteka gari lenu wote mkaambiwa mtoe simu zenu, wewe ukatoa NOKIA tochi na kumuhakikishia jambazi kuwa ndio simu unayoitegemea, mara Blacberry Bold uliyoificha kwenye chupi ikaanza kulia
 UTAJUA KUWA MUDA UMEFIKA pale ambapo unawasha kiberiti kucheki kama kuna mafuta kwenye jenereta iliyozima ghafla
UTAJUA KUWA MUDA UMEFIKA pale mpenzi wako anapokwambia, “Ingia uvunguni mwa kitanda mume/mke wangu kaja”. Wakati uko uvunguni simu yako ya Mchina inaanza kuita

Comments