PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

UKIKOHOA TU UMEHARISHA OHOOO

Jamaa aliajiriwa kwenye famasi, tatizo lake alikuwa msahaulifu sana, kila mteja akija kutafuta dawa, anajikuta kasahau imewekwa wapi, ikawa kazi yake iko hatarini. Siku moja kaja mteja anakohoa, akatafuta dawa ya kikohozi hakuipata akachukua dawa ya kufungua tumbo akamkabidhi mgonjwa tena akamwambia anywe pale pale chupa nzima kisha akamruhusu aende, mgonjwa hakwenda mbali, katembea kidogo kisha akaegemea nguzo ya umeme. Muda mchache baadae bosi wake akamuuliza kama ameuza chochote;
JAMAA: Ndio kuna mteja alikuja anakohoa nikatafuta dawa ya kikohozi sikuipata nimemuuzia dawa ya kufungua tumbo.
BOSI: Hiyo dawa kamwe haiponyeshi kifua
JAMAA: Najua haiponyeshi lakini inazuia, si unaona mgonjwa yule pale kaegamia nguzo, toka kanywa dawa anaogopa kukohoa

Comments