HATUPIMI BANDO

18 December 2012

NINI SIYO FEKI?

Okay okay okay Chekanakitime imemaliza kusoma gazeti moja na haya ndio matokeo. Katika gazeti moja kuna vichwa vya habari hivi hapa;
1. Majaji walalamikia uchakachuaji wa pensheni -uk 3
2. Serikali yachunguza vyuo feki -uk 5
3. Kuingizwa kwa bidhaa feki Wizara ibebe lawama - uk 6
4. Wadai 'helmet' hazina viwango -uk 9
5. Mbaroni kwa tuhuma za kuhodhi fedha bandia - 13
Ni wazi nchi hii vitu feki vimejaa kila kona, je, hili jua sio feki nalo? Mimi mwenyewe je? Rafiki zangu? Duu aise, je we msomaji?

No comments: