HATUPIMI BANDO

10 December 2012

NANI KAMUUA CHIEF MKWAWA?

MWALIMU: Nani alimuuwa Chifu Mkwawa?
MWANAFUNZI 1; Sio mimi
MWANAFUNZI 2: Jana sikuja shule
MWANAFUNZI 3:Mwalimu kwa kweli sie unatuonea....baada ya mwalimu kuona darasa zima ni vilaza akaamua kumtaarifu mwalimu mkuu kuwa darasa zima wanashindwa kumtaja aliyemuuwa Chief Mkwawa, ambaye naye akaja kwa ukali
MWALIMU MKUU: Nani aliyemuua Chifu Mkwawa? Msipojibu humu ndani patawaka moto...darasa zima wakaanza kulia
DARASA:Mwalimu sio sisi
Mwalimu Mkuu akamgeukia mwalimu wake;
MWALIMU MKUU: Mwalimu una uhakika huyu muuwaji yuko darasa hili?

No comments: