PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

MERRY NEW YEAR TO YOU TOO ALSO PIA NAWE

Kwa kusema kweli NIMEPATA SHOCK.......sikutegemea kabisa na wala sikufikiria wala kuwaza wala kuota unaonaee. Ila nashukuru Xmas hii imenifungua macho masikio na mawazo. Kumbe asilimia kubwa ya rafiki zangu ambao kila siku tulikuwa tukiwasiliana kupitia txt za simu na hapa FB kwa Kiswahili kumbe ni mahiri wa Kiingereza umeonaee. Sijui kwanini walikuwa wananificha uwezo wao huo. Asilimia 98.34 ya salamu za Xmass nilizopata zimeandikwa Kiingereza, jambo ambalo limenifanya niweze kutetea popote duniani kuwa nchi yangu Kiingereza ni lugha ya kawaida kabisa mtaani si unaonaee. Japokuwa salamu nyingine zilikuwa zinanishangaza kidogo maana mwisho unakuta zimemalizika kwa jina la mtu mwingine siyo yule aliyenitumia , lakini hilo siyo ishu UNAONAEE. Nangojea za I wish you merry new year, si ndio ee?

Comments