HATUPIMI BANDO

26 December 2012

MALIPO KABURINI

Jamaa alikuwa anaishi karibu na makaburi, basi akajigundulia njia ya kupata usafiri bila kilipa, akawa kila akikodi bodaboda na bajaji alikuwa anaomba kuachwa makaburini. Katikati ya safari akawa anafutika pamba kwenye pua zake wakati wa kushuka anaongea kwa kubana pua,'Nimefika home unanidai shilingi ngapi?' madereva wote wa bodaboda na bajaji walikuwa wanatoka nduki. Siku moja akafanya mchezo huyo kwa dereva mmoja wa bodaboda, walipofika mwisho wa safari dereva wa bodaboda hakutishika na pamba akakomaa anataka nauli yake.
JAMAA: Ok basi twende kwenye kaburi langu nikakupe
BAJAJI: Twende....walipofika kaburi fulani, jamaa akagonga msalaba.
JAMAA: Wakulu, wakulu fungueni nipeni alfu nane huyu jamaa ananidai nauli......ghafla mkono mrefu ukatoka kaburini ukiwa umeshika noti mkononi....ASUBUHI KULIKUTWA PEA MBILI ZA VIATU KANDO YA KABURI, NA KIBAJAJI KANDO YA MAKABURI

No comments: