HATUPIMI BANDO

3 December 2012

KUJUA KUSOMA USUMBUFU


Dah kumbe kujua kusoma sio lazima faida. Tena mara nyingine ni hasara. We fikiria uko katikati ya mji, unataka kujisaidia, hakuna choo cha umma, unaona kakichochoro fulani uawahi unataka kujisaidi unakuta maandishi makubwa, USIKOJOE HAPA. Unakuwa mdogooo, ungekuwa huji kusoma wala isingekusumbua,ungemaliza shughuli yako na kutoka mwepesiiii. Una shida na mtu, unamfuata kazini kwake unakuta kibao kimeandikwa usiingie hapa, unabaki umezubaa nje unasubiri namna ya kuomba ruksa uingie, ungekuwa hujui kusoma ungeingia na kumaliza ishu zako na kusepa. Sababu tummejua kusoma, vibao hivi vya usikae hapa, usipite hapo, hakuna kazi, mbwa mkali, nyumba hii inalindwa na umeme, vinatufanya tuwe waoga hata kama hakuna kitu. Iko haja ya kuanzisha shule ya kufuta kujua kusoma na kuandika. Hii mifesbuk wala isingekuwa ishu

No comments: