PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

JAMAA ATAGA MAYAI

Jamaa katoka ulevini kalewa sana kama kawaida, akanyata chumbani kwake, ili mkewe asiamke akaingia ndani ya shuka, haikuchukua muda akawa katika uingizi mzito. Ghafla akaamka akakuta kumesha kucha, ila kitu cha ajabu akakuta pembeni yake kuna mwanaume badala ya mkewe. Akamuuliza yule mwanaume, "We nani na umekujaje chumbani kwangu?". Yule mwanaume akacheka sana,'Hahahahahaha chumbani kwako? Hapa si chumbani kwako hapa ni ahera, na mimi ndie shetani mkuu Lusifa". Jamaa, "Una maana nimeshakufa?", 'Haswaaa, toka ulipotoka ulevini jana". Jamaa akakaanza kulia na kulalamika," Haiwezekani jamani mi bado kijana kuna mambo mengi nilikuwa sijamaliza, chonde chonde Mzee Lusifa nirudishe duniani japo mwaka mmoja". Lusifa akamuangalia jamaa kisha akamwambia ,"Okay lakini huwezi kurudi duniani kama binadamu, labda urudi kama kuku au panya au mjusi" Jamaa akachagua kurudi kama kuku. Basi fumba na kufumbua akajikuta yuko duniani akiwa na kuku wenzie kwenye banda. Akawa kajikunyata hajui hata aanzie wapi, ghafla akajisikia hali ya aajabu akajua anahisi kutaga yai. Akajivuta pembeni kwenye kona, na kuanza kujikamua kwa nguvu, yai la kwanza likatoka, akajisikia nafuu, kisha akajikuta anataka kutaga la pili akajikamua kwa nguvu huku akitetea, yai la pili likatoka....na ndipo hapo aliposikia kofi la nguvu shavuni na sauti ya mkewe ikifuatia,"Mshenzi mkubwa wewe, ulevi wako sasa mpaka unakunya kitandani zoa uchafu wako haraka"

Comments