HATUPIMI BANDO

29 December 2012

CHA WIKI ENDI

Ilikuwa Jumamosi asubuhi, kazee kamjini kakaingia na bonge ya mdada kwenye yard ya magari mapya.
KAZEE: Chagua gari unalotaka mpenzi....kabinti kakazunguka na kwa msaada wa mwenye wa mwenye yard kakapata Noah nyeupe nzuri sana.
MDADA: Mi naitaka hii
KAZEE: Hakuna tatizo kabisaaa. Kwani shilingi ngapi hii? Kakatoa kitabu cha cheki na kuandika cheki palepale na kumpa mwenye yard
MUUZAJI: Sasa mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu nikihakikisha kuwa una pesa benki. Nipe namba yako ya simu Mzee
KAZEE: Hilo nilijua. Hay twende zetu sweety Jumatatu ntakuja kukuchukulia gari lako..................Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.
MUUZAJI: We mzee kavu sana, akaunti yako ilikuwa haina hata senti tano.
KAZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.

No comments: