HATUPIMI BANDO

1 December 2012

BABA HIZO ZA NINI?

1st December-siku ya ukimwi duniani-
Mzee anaejiita wa kisasa alienda na mwanae famasi kununua kondom. Alipoulizia akajibiwa ziko za viboksi vyenye kondom  tatutau, sitasita na zilizo fungwa 12 kwa paketi;
DOGO: Baba hizo za nini?
BABA: Hizi zinaitwa kondom, huzuia maambukizi ya UKIMWI wakati wa kujamiiana.
DOGO: Kweli hata sisi tulifundishwa shuleni, sasa mbona zinafungwa kwa paketi tofauti?
BABA: Hizo zilizofungwa 3, kwa ajili ya vijana wanaopenda kwenda klabu wikiendi. Moja ya Ijumaa, nyingine Jumamosi na ya tatu Jumapili. Zile sitasita ni kwa ajili ya wale wenye nyumba ndogo, mbili Ijumaa, mbili Jumamosi mbila Jumapili. Hizi za kumi na mbili ni za walio katika ndoa, ya kwanza Januari, ya pili Februari hivyohivyo mpaka mwaka unaisha.

No comments: