HATUPIMI BANDO

31 December 2012

DAR HAPO KALE

Posta ya zamani

Nkrumah Street

Salender Bridge

Tanzania Legion

Mtaa wa Uhuru

WAKULU LEO NDIO SIKU ILE YA DIJITALI MI NIKO TAYARI


30 December 2012

ZA MWISHO WA MWAKA -3- ANAMEREMEMETAAA


ZA MWISHO WA MWAKA -2-UTARUDIA TENA KWENDA NYUMBA NDOGO?


ZA MWISHO WA MWAKA -1 ANANIAMSHA

MWANAMIMI:Dokta tatizo langu kubwa sana
DOKTA: Nini tena?
MWANAMIMI: Usiku tukiwa faraga na mume wangu, huwa anapiga sana kelele
DOKTA: Lakini mama hilo ni jambo la kawaida
MWANAMIMI: Hapana ananisumbua, kelele zake huwa zinaniamsha usingizini

WATOTO WENGINE UTUNDU UMEZIDI


SHENZI TYPE UNACHEZEA KUOLEWA NA MWAFRIKA WEWE


DECEMBER 31, TUNAHAMIA DIJITALI

Nasikitika kukutaarifu kuwa elimu yako yote uliopata ipo kwenye mfumo wa analogia, kwa hiyo kufikia Desemba 31, ulivyosoma vyote vitafutika kwani  mfumo huo unazimwa na mfumo wa dijitali unawashwa. Ili uingie katika mfumo  wa dijitali, wahi kujiandikisha chechekea kabla shule hazijaanza

MKUTANISHE NA NYUMBA NDOGO

KASONGO: Nataka nimpe mke wangu bonge ya suprise mwaka mpya, sijui nimfanyie nini?
DEVI: Mkutanishe na nyumba ndogo yako

NAOMBA UNGA

OMBAOMBA kagonga mlango wa Mzee Juma;
OMBAOMBA: Mzee naomba mia tano
MZEE JUMA: Sina
OMBAOMBA: Naomba basi unga kidogo nikapike ugali
MZEE JUMA: Sina
OMBAOMBA: Naomba japo shati bovu
MZEE JUMA: Sina
OMBAOMBA: Basi tusindikizane tukaombe wote huko mbele

29 December 2012

HUYU SI NILIMUONA LIDAZ JUZIJUZI?


NGOJA TUTIBU PUA KWANZA

KIBABU:Dokta nina tatizo sijui ni uzee au nini lakini kila mara najambajamba hovyo, ila uzuri wake ushuzi haunuki wala hautoi sauti
DOKTA: Eti ehhh
KIBABU: Hata hapa nimeshafutua mara tatu humu ofisini kwako
DOKTA: haya chukua hivi vidonge umeze halafu urudi wiki ijayo
KIBABU: Ntakuwa nimepona?
DOKTA: Vidonge vitazibua pua zako, maana zinashindwa kunusa, wiki ijayo ntakupa vidonge uzibue masikio, halafu tutapima kwanini unajambajamba hovyo

CHA WIKI ENDI

Ilikuwa Jumamosi asubuhi, kazee kamjini kakaingia na bonge ya mdada kwenye yard ya magari mapya.
KAZEE: Chagua gari unalotaka mpenzi....kabinti kakazunguka na kwa msaada wa mwenye wa mwenye yard kakapata Noah nyeupe nzuri sana.
MDADA: Mi naitaka hii
KAZEE: Hakuna tatizo kabisaaa. Kwani shilingi ngapi hii? Kakatoa kitabu cha cheki na kuandika cheki palepale na kumpa mwenye yard
MUUZAJI: Sasa mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu nikihakikisha kuwa una pesa benki. Nipe namba yako ya simu Mzee
KAZEE: Hilo nilijua. Hay twende zetu sweety Jumatatu ntakuja kukuchukulia gari lako..................Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.
MUUZAJI: We mzee kavu sana, akaunti yako ilikuwa haina hata senti tano.
KAZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.

WATU WANA KIPAJI CHA KUZALIWA


28 December 2012

BAADA YA KUONA KIMINI CHA NGUVU AKAJUA...........

Mdada mmoja mrembo sana alikuwa kapewa talaka na mumewe akahamia nyumba aliyokuwa kapanga  DEVI. DEVI alipomuona mpangaji mpya roho yote ikamtoka. Akajitahidi kila njia kumuonyesha kuwa nae yupo na ni bachela, mdada akawa anaendelea na shughuli zake bila hata kuonyesha dalili za kumwona DEVI. Jioni moja DEVI akiwa kapumzika akasikia hodi kwenye chumba chake, alipofungua akakutana uso kwa uso na mdada mpangaji, kapendeza sana na akiwa kavaa kimini cha nguvu;
MDADA: Samahani kaka Devi, yaani nimekaa muda mrefu mpweke nimeona leo lazima nitoke nikajirushe kidogo kisha nipate bwana niondoe uchovu. Vipi we uko free?
DEVI: Mimi sana tu niko free sina kitu chochote ninachofanya jioni hii, yaani niko free kabisa si unaona mwenyewe niko free sina ishu kabisaaa
MDADA: Loh nakushukuru sana kaka yangu, basi ngoja nikuletee watoto wangu ushinde nao mpaka ntakaporudi

26 December 2012

BOSI WA KITAA


MAFALA WAO HAHAHAHAHAHAHA

KAKA P: Oyaa ukiwa faraga na mkeo uwe unafunga pazia jana usiku mtaa mzima ulikuwa unakuchungulia, watu wote wanakucheka
Mzee D: Hahahahaha wao ndio mafala, jana mie nilikuwa safariWE ONDOKA ZAKO

Mdada alikuwa anajua kuwa mumewe yuko safari akamkaribisha mpenzi kwake, kwenye saa 6 usiku mumewe akapiga hodi, mdada akamwambia mpenzi simama hapo pembeni jifanye sanamu mengine niachie. Jamaa akasimama kama sanamu mke akamfungulia mumewe na kumpokea mizigo na kumkaribisha ndani. Mume akamuangalia yule jamaa kisha akamuuliza mkewe,' Nini hiki?'. Mke akajibu,' Wamachinga walipita na masanamu wanauza na mimi nikanunua moja'. Mume akajibu ,'OK'. Jamaa akala akalala, kwenye saa 9 usiku akaamka, akaliendea lile sanamu akaliambia,'Pole kwa mbu ndugu yangu, heri uondoke zako mie mwenzio ishu kama hii imenikuta Iringa nikapigwa na baridi siku mbili ndio nikaweza kuondoka. Haya usiku mwema'

MALIPO KABURINI

Jamaa alikuwa anaishi karibu na makaburi, basi akajigundulia njia ya kupata usafiri bila kilipa, akawa kila akikodi bodaboda na bajaji alikuwa anaomba kuachwa makaburini. Katikati ya safari akawa anafutika pamba kwenye pua zake wakati wa kushuka anaongea kwa kubana pua,'Nimefika home unanidai shilingi ngapi?' madereva wote wa bodaboda na bajaji walikuwa wanatoka nduki. Siku moja akafanya mchezo huyo kwa dereva mmoja wa bodaboda, walipofika mwisho wa safari dereva wa bodaboda hakutishika na pamba akakomaa anataka nauli yake.
JAMAA: Ok basi twende kwenye kaburi langu nikakupe
BAJAJI: Twende....walipofika kaburi fulani, jamaa akagonga msalaba.
JAMAA: Wakulu, wakulu fungueni nipeni alfu nane huyu jamaa ananidai nauli......ghafla mkono mrefu ukatoka kaburini ukiwa umeshika noti mkononi....ASUBUHI KULIKUTWA PEA MBILI ZA VIATU KANDO YA KABURI, NA KIBAJAJI KANDO YA MAKABURI

25 December 2012

MERRY NEW YEAR TO YOU TOO ALSO PIA NAWE

Kwa kusema kweli NIMEPATA SHOCK.......sikutegemea kabisa na wala sikufikiria wala kuwaza wala kuota unaonaee. Ila nashukuru Xmas hii imenifungua macho masikio na mawazo. Kumbe asilimia kubwa ya rafiki zangu ambao kila siku tulikuwa tukiwasiliana kupitia txt za simu na hapa FB kwa Kiswahili kumbe ni mahiri wa Kiingereza umeonaee. Sijui kwanini walikuwa wananificha uwezo wao huo. Asilimia 98.34 ya salamu za Xmass nilizopata zimeandikwa Kiingereza, jambo ambalo limenifanya niweze kutetea popote duniani kuwa nchi yangu Kiingereza ni lugha ya kawaida kabisa mtaani si unaonaee. Japokuwa salamu nyingine zilikuwa zinanishangaza kidogo maana mwisho unakuta zimemalizika kwa jina la mtu mwingine siyo yule aliyenitumia , lakini hilo siyo ishu UNAONAEE. Nangojea za I wish you merry new year, si ndio ee?

PICHA FUNGA MWAKA TOKA GAZETI LA UHURU


24 December 2012

MBILI KWA MPIGO

                                 1
DOGO: Eti mama malaika huwa wanapaa?
MAMA: Ndio malaika wanapaa, kwanini unauliza?
DOGO:Baba alimuita dada Malaika, dada atapaa?
MAMA: Ndio atapaa leoleo kurudi kijijini kwao

                                   2 

GULO: Bebi simu yako nzuri umepata wapi?
DEVI: Nilishinda kwenye mashindano
GULO: Mashindano ya nini Bebi?
DEVI: Mashindano ya mbio, kati yangu, mwenye simu, polisi na wananchi wenye hasira kali.

GETI LIKO WAZI

Baada ya kukaa miaka mingi katika hospital ya machizi, chizi mmoja akaamua lazima atoroke. Akaanza kufanya mazoezi ya kuruka geti. Kila siku akawa anafanya mazoezi ya nguvu, hatimae akafikia muda akawa na uwezo wa kuruka geti na kutoroka. Siku ya kuondoka akawaaga wenzie kuwa anaenda kuruka geti atoroke. Akaaondoka, dakika kumi baadae akarudi, wenzie wakamuuliza,'Vipi umeshindwa kutoka?' Akajibu "Hapana, ntajaribu tena kesho. Leo nimeenda nimeshindwa kuruka maana geti wameacha wazi"

MTOTO WANGU BADO MDOGO

MZAZI: Kwanini umemfukuza mtoto wangu shule?
MWALIMU: Mtoto wako kanishinda hawezi hata kusema spelling za tembo
MZAZI: Mwalimu sasa huo uonezi, mtoto wangu bado mdogo, si umuulize spelling za vitu vidogo kama sisimizi,nyenyere

UTAJUAJE KAMA SIKU YAKO YA KIFO IMEFIKA?


Si rahisi kujua siku yako ya kifo, lakini kuna watu hupata bahati ya kujua muda umefika. Hapa ni baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia kujua kuwa saa yako ya kifo imewadia…..
UTAJUA KUWA MUDA UMEFIKA..pale ambapo majambazi wenye silaha wameteka gari lenu wote mkaambiwa mtoe simu zenu, wewe ukatoa NOKIA tochi na kumuhakikishia jambazi kuwa ndio simu unayoitegemea, mara Blacberry Bold uliyoificha kwenye chupi ikaanza kulia
 UTAJUA KUWA MUDA UMEFIKA pale ambapo unawasha kiberiti kucheki kama kuna mafuta kwenye jenereta iliyozima ghafla
UTAJUA KUWA MUDA UMEFIKA pale mpenzi wako anapokwambia, “Ingia uvunguni mwa kitanda mume/mke wangu kaja”. Wakati uko uvunguni simu yako ya Mchina inaanza kuita

21 December 2012

BREAKING NEWSSSS--TANZANIA HAKUNA RUSHWA KABISAAA

BAADA YA SHUTUMA ZA MUDA MREFU KUTOKA PANDE NYINGI ZA DUNIA, HATIMAE KAMPUNI MOJA KUTOKA INDIA IMEFANYA UTAFITI AMBAO JIBU LAKE LITAZIKATA KILIMILIMI NCHI ZA SKANDINAVIA. UTAFITI UMEONYESHA KUWA KWELI ZAMANI TANZANIA ILIKUWA NA MCHEZO WA RUSHWA, LAKINI KWA SASA WATU WAMEBADILIKA HAKUNA ANAETOA WALA KUPOKEA RUSHWA HATA KIDOGO. KAMPUNI HII IMEJARIBU KUFUATIA NYENDO ZA TRAFIKI KWA MWEZI MZIMA NA KUKUTA WATU HAWA NI WENYE ROHO NYEUPE KAMA NGUO ZAO, NA MADAKTARI NA MANESI PIA NAO PIA WEUPE. MAHAKAMA ZETU ZIMESIFIWA SANA KWA KUWA NI ZA KUIGWA KWA UADILIFU...TANZANIA IS CORRUPTION FREE...AU FREE CORRUPTION?

MI SILI HUKU

Jamaa alikuwa kaishiwa hivyo akashindwa kwenda kula kwenye hoteli ya bei ya juu, akakatisha vichochoro akaingia kwa mama ntilie mmoja akaigiza chakula. Akashangaa jamaa aliyemletea chakula ni jamaa walisoma nae mpaka chuo.
JAMAA 1: Duh aise kumbe unafanya huku, vipi huoni aibu kusoma kote unafanya kazi huku?
JAMAA 2:  Mi huku nafanya kazi tu lakini kula sili huku

20 December 2012

WEKA FANTA BARIDI

Mtoto kapelekwa hospitali na mdingi wake, dokta akawa anamuandikia dawa, mara baba yake akatoka nje kuongea na simu. Mtoto akamuinamia daktari akamwambia kwa sauti ya chini chini, 'Dokta kwenye dozi andika Fanta Baridi,chips na kuku kila siku kwa siku 30,kutwa mara tatu'

NIMEMEZA FUNGUO

MJUKUU: Nimemeza funguo wa mlango wa chumba changu
DOKTA : Lini?
MJUKUU: kama miezi mitatu iliyopita
DOKTA: Sasa mbona unakuja leo?
MJUKUU: Nilikuwa na funguo ya ziada sasa leo nayo nimeipoteza

UNAJUA MICROSOFT OFFICE

BOSS: Nasikia unatafuta kazi, kompyuta unajua?
MJAMAA: Sana tu mzee
BOSS: Unajua Microsoft Office?
MJAMAA: Msema kweli mpenzi wa Mungu, siijui lakini mkinielekeza iko mtaa gani ntafika tu Mzee.

19 December 2012

JANA NIMEKUOTA

MDADA: Swrty jana nimekuota
MKAKA: Umeota nini?, Niko na wewe?
MDADA: Hapana nimeota tuko kwenye daladala, ghafla likapinduka likatumbukia mtoni. Ukaanza kuogelea unatapatapa
MKAKA: Ntakuwa nilikuwa nakutafuta mpenzi wangu
MDADA: A wapi ulikuwa unapiga kelele,'Konda leta chenji yangu, konda mia mbili yangu'

MAPENZI NA KIFO

Unajua maana halisi ya KIFO na MAPENZI?
MAPENZI-ni pale mume anapomfumania mkewe gesti na mwananume mwingine, na kwa upole anamwambia mkewe,' Vaa nguo swity twende zetu nyumbani'. 
KIFO- Ni pale mke anapokubali kumfuata mumewe nyumbani

18 December 2012

NINI SIYO FEKI?

Okay okay okay Chekanakitime imemaliza kusoma gazeti moja na haya ndio matokeo. Katika gazeti moja kuna vichwa vya habari hivi hapa;
1. Majaji walalamikia uchakachuaji wa pensheni -uk 3
2. Serikali yachunguza vyuo feki -uk 5
3. Kuingizwa kwa bidhaa feki Wizara ibebe lawama - uk 6
4. Wadai 'helmet' hazina viwango -uk 9
5. Mbaroni kwa tuhuma za kuhodhi fedha bandia - 13
Ni wazi nchi hii vitu feki vimejaa kila kona, je, hili jua sio feki nalo? Mimi mwenyewe je? Rafiki zangu? Duu aise, je we msomaji?

NAWATAKIA KRISMAS NJEMA KAMA WENGINE


17 December 2012

JE ULIFELI? PATA NAFASI ZA KAZI YA UANDISHI

KAZI KAZI KAZI JOB JOBLESS...Blog yako maarufu ya www.chekanakitime.blogspot.com itaanza mwaka 2013 kwa kutoa taarifa mbalimbali za mambo yanayotokea na yasiyotokea hapa nchini na hata kote duniani na ulimwenguni. Ili kufanikisha azma hiyo kunahitajika waandishi wasio mahiri na waliofeli kozi za uandishi. Hii inatokana na kuwa wale waandishi waliopata bahati ya kupasi tunaona kila siku kazi zao ka
tika vyombo vyetu vya habari, sasa tungetaka kutoa nafasi kwa wale waliopata nafasi ya kufeli ili nao tuone umahiri wao uliosababisha wakaweza kufeli. Kazi hii ambayo haitakuwa na mshahara ili tuwe tofauti zaidi na hawa waliopasi inaanza mara moja,kazi kwako ni kuni inbox maombi ya kazi unashauriwa usitaje jina lako la ukweli ohhooo, stori nyingine ukileta zinaweza kusababisha ukong'otwe mtaani kwenu au ulogwe na wasanii au Wakurugenzi wa mashirika unayotaka kuwaumbua. Haya kazi kwenu vilaza. Kama Mama K anavyosemaga Equal Opportunity For All, hapo najua mmetoka kapa tafsiri yake ni hata mafala wapewe chansi

Breaking Newsssssss- HAKUNA MGAO

Toka kushoto; Mimi, Bada C Ugali(msemaji mkuu Afrika), Don Othman(mpiga picha), Totoo(mcheza show wa shirika), Waandishi wa Habari, Mstari wa nyuma Wasomaji wa habari

Waheshimiwa waandishi, waheshimiwa wapiga picha za mnato, waheshimiwa wapiga picha za video, waheshimiwa makanjanja, waheshimiwa mabibi na mabwana. Kwanza naomba nichukue nafsi hii kuwaombeni radhi kwa hali iliyopo hii ni kutokana na kuanguka kwa transfoma moja ambayo watoto wa Uswahilini waliipiga mawe jana asubuhi. Lakini tatizo hilo linashughulikiwa na mafundi wetu mahiri.
Leo shirika limenituma nije kuongea na nyinyi ili kuondoa uvundo, samahani uvumi ulioenea kwenye vyombo vya habari vya ndani, nje na hata pembeni yetu na pia kwenye mitandao ya kijamii na isiyo ya kijamii kuhusu utendaji wa shirika letu, na hivyo kuchafua jina tukufu la shirika letu la  Ugavi wa Giza. Mnaonaee
Awali ya yote nichukue nafasi hii kumpongeza Rais wetu kwa kushinda kwa kishindo katika uchaguzi uliopita, pia nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri wetu kwa ukakamavu wa hali ya juu kusimamia mishahara  na marupurupu yetu wakati wa Bunge lililopita. Mheshimiwa Waziri take it from me wafanyakazi wote na wake zao wanakupenda ile mbaya unaonaeee.
Baada ya hayo nirudi kwenye mada. Katika siku za karibuni kumetokea kundi la watu wasiopenda maendeleo, wapinzani wa juhudi zetu ambao wamesimama kidete kulaani na kubeza juhudi zetu za kuimarisha sekta hii ya giza. Uwongo mkuu wanotumia ni kuwadanganya wananchi wenye nia njema eti kuna mgao wa giza. Ndugu waandishi nyinyi wenyewe mtakubaliana na mimi baada ya kuwagawieni mshiko wenu mwisho wa kikao kuwa huu ni uwongo wa wazi. Au siyoooo?
Kinachotokea hapa si mgao hata kidogo, bali ni matatizo ya kiufundi ambayo yanatokana na sababu mbalimbali, kwa mfano hali tuliyonayo hapa ni kosa la watoto waliopiga manati transfoma, ikatikisika katika vibration chamber, jambo lililokoz internal bleeding ya oilcom, hapo kilichotokea ni zile Read Only Memory kukatika na kusababisha kutrip kwa excel,iliyoangusha transformer na kusababisha kinachoonekana mgao. Katika sehemu nyinge kweli kumefanyika downloading kubwa kwenye hizi internet café ambazo zimezagaa bila mpango, sasa kuna vijana wamedownload gigabyte nyingi mno hivyo kukoz internal hameorage ya system na kuonekana eti ni mgao. Wananchi wenzangu tuache hi dhana potofu ya kuhisi kitu. Ukweli ni kuwa mkipunguza kudownload kwenye hizo internet café nchi nzima haitakuwa na mgao wa giza. Otherwise tutaendelea kulaumiana.
Pia niongelee hili swala la kununua kuni za matumizi ya kampuni yetu  nje ya nchi wakati huku kwetu kuni ziko, jamani this is biznes, na katika bizness, kuna balance sheet, profit and loss account, kitaalamu balance sheet, msichanganye hii na bed sheet, ni kitu muhimu sana kuangalia, kwa sababu matokeo yake yanakuja onekana kwenye profit and loss account. Tujiulize hivi ukijiuzia mwenyewe , how are you going to balance sheet? Tusiwe wepesi tu kutamka , ni muhimu kuwa na client wa kutoka nje ambaye kwenye accounts zetu hujulikana kama external account, ambapo biashara hii inakuwa na sura ya kimataifa zaidi. There fore kununua kuni nje ni kuimarisha biashara kimataifa zaidi, we are making a name of ourselves and the Nation. Kampuni inakuwa ni ya kimataifa zaidi. Tushirikiane kwa nguvu zote kutetea kuni za njee, ili zetu nazo ziuzwe nje baada ya kukosa soko la ndani unaonaee. Ndugu waandishi baada ya mkutano huu wote mkachukue kabahasha kadogo ka laki sita sita za nauli ya kuwafikisha kwenye ofisi zenu, tukiwa pamoja nchi itaendelea.
Kauli mbiu yetu ni giza ni mali, bila giza hakuna tochi, bila giza hakuna jenereta, giza hoyeeeeeeeeeeeeeeeee

16 December 2012

SWALI , UNGEKUWA WEWE UNGEFANYAJE?

Umepata mpenzi mpya unaona ujikakamue umtoe out. Mnaingia mahala pa nguvu, anakula anakunywa vizuri sana hatimae unafika muda kuondoka, anakwambia kuwa atalazimika kurudi kwao maana baba yake mkali, unajichekelesha na kutoa hela yako ya mwisho kumlipia taxi inabakia na mia tatu za daladala kwenda kwako. Unamuaga kuwa kuna biznes patna jirani unaenda kudiskas nae biashara yenu, unakula kona na kwenda subiri daladala. Hatimae gari linafika unaingia ndani na kwa mshangao unamkuta mpenzi nae kumbe kaminya mkwanja kaamua kupanda daladala, unafanyaje?

BEES IN AMERICA

TEACHER: Ok class what do you call a bee in America?
DEVI: USB

MKOROGO WA WIKI


15 December 2012

NIKO NA WAGENI TOKA BULGARIA

MKE: Haloo mume wangu uko wapi saa hizi?
MUME: Aise sori mke wangu niko bizi sana, niko ofisini tuna wageni kutoka Bulgaria, we are very busy. Vipi we uko wapi my dear?
MKE; Niko meza ya nyuma yako hapa Corner Bar, naomba na mimi Amarula kama anayokunywa mgeni wako toka Bulgaria

14 December 2012

BANGI MBAYA JAMANI HAMSIKIAGI?


ORIJINAL KOMEDI

UKIENDA MOTONI UTAKUWA BIZI

Katika maisha kuna vitu viwili muhimu kuwaza,
Aidha wewe umzima au unaumwa;

Kama umzima hakuna la kuwaza,
Lakini kama unaumwa kuna vitu viwili vya kuwaza
Aidha utapona au utakufa,

Ukipona hakuna la kuwaza,
Ukifa, kuna mambo mawili ya kuwaza,
Aidha unaenda mbinguni au unaenda motoni,
Ukienda mbinguni hakuna la kuwaza,
Lakini ukienda motoni, utakuwa bizi unawasalimia ndugu na marafiki, huku ukiwashangaa masupastaa NA WAREMBO WA NGUVU waliojazana huko, utakuwa huna muda wa kuwaza lolote jingine

13 December 2012

MKE WANGU ALINIKUTA

JAMAA kaingia kituo cha polisi huku anavuja damu kichwani;
POLISI: Nini tena wewe?
JAMAA: Naomba PF3 nikapate matibabu
POLISI: Umefanya nini?
JAMAA: Nimepasuka kichwa
POLISI: Umepasukaje kichwa?
JAMAA: Nilikuwa nambusu mpenzi wangu
POLISI:Toka lini ukibusu mpenzi unapasuka kichwa?
JAMAA: Mke wangu alinikuta nambusu

KUCHORA TATOO INATAKA MOYO ohoo


12 December 2012

CHAKUBANGA TENA
JAMAA ATAGA MAYAI

Jamaa katoka ulevini kalewa sana kama kawaida, akanyata chumbani kwake, ili mkewe asiamke akaingia ndani ya shuka, haikuchukua muda akawa katika uingizi mzito. Ghafla akaamka akakuta kumesha kucha, ila kitu cha ajabu akakuta pembeni yake kuna mwanaume badala ya mkewe. Akamuuliza yule mwanaume, "We nani na umekujaje chumbani kwangu?". Yule mwanaume akacheka sana,'Hahahahahaha chumbani kwako? Hapa si chumbani kwako hapa ni ahera, na mimi ndie shetani mkuu Lusifa". Jamaa, "Una maana nimeshakufa?", 'Haswaaa, toka ulipotoka ulevini jana". Jamaa akakaanza kulia na kulalamika," Haiwezekani jamani mi bado kijana kuna mambo mengi nilikuwa sijamaliza, chonde chonde Mzee Lusifa nirudishe duniani japo mwaka mmoja". Lusifa akamuangalia jamaa kisha akamwambia ,"Okay lakini huwezi kurudi duniani kama binadamu, labda urudi kama kuku au panya au mjusi" Jamaa akachagua kurudi kama kuku. Basi fumba na kufumbua akajikuta yuko duniani akiwa na kuku wenzie kwenye banda. Akawa kajikunyata hajui hata aanzie wapi, ghafla akajisikia hali ya aajabu akajua anahisi kutaga yai. Akajivuta pembeni kwenye kona, na kuanza kujikamua kwa nguvu, yai la kwanza likatoka, akajisikia nafuu, kisha akajikuta anataka kutaga la pili akajikamua kwa nguvu huku akitetea, yai la pili likatoka....na ndipo hapo aliposikia kofi la nguvu shavuni na sauti ya mkewe ikifuatia,"Mshenzi mkubwa wewe, ulevi wako sasa mpaka unakunya kitandani zoa uchafu wako haraka"

10 December 2012

NANI KAMUUA CHIEF MKWAWA?

MWALIMU: Nani alimuuwa Chifu Mkwawa?
MWANAFUNZI 1; Sio mimi
MWANAFUNZI 2: Jana sikuja shule
MWANAFUNZI 3:Mwalimu kwa kweli sie unatuonea....baada ya mwalimu kuona darasa zima ni vilaza akaamua kumtaarifu mwalimu mkuu kuwa darasa zima wanashindwa kumtaja aliyemuuwa Chief Mkwawa, ambaye naye akaja kwa ukali
MWALIMU MKUU: Nani aliyemuua Chifu Mkwawa? Msipojibu humu ndani patawaka moto...darasa zima wakaanza kulia
DARASA:Mwalimu sio sisi
Mwalimu Mkuu akamgeukia mwalimu wake;
MWALIMU MKUU: Mwalimu una uhakika huyu muuwaji yuko darasa hili?

7 December 2012

HAYA MOMBASA NAKO WATAKA HAKI ZAOOO

NI WAKATI WA MAZOEZIIIIIIIIIIII

MWANASHERIA MKWARE

Mwanasheria mmoja mkware alitumia gari yake kama gest, mpenzi wake akasahau nguo ya ndani kwenye gari. Kesho yake mke wa mwanasheria akaikuta ile nguo, kwa hasira akaichanachana na kumfuata jamaa na kumtupia usoni. MWANASHERIA: Mke wangu umefanya nini sasa? Chupi hii ilikuwa ushahidi muhimu wa kesi ambapo mteja wangu tajiri sana amebakwa na mfanya biashara maarufu, na tungepata fedha nyingi sana kupitia kesi hii sasa wewe umeharibu ushahidi, My God, what do I do?
MKE: Mume wangu samahani sikutumia akili ni wivu tu samahani sana sirudii tena
MWANASHERIA:Its okay lakini umenirudisha nyuma sana kikazi

NIPE KONDOM SAIZ NDOGO

Babu kaingia chumba cha mjukuu wake kakuta kondom kwenye meza;
BABU: Hiki nini?
MJUKUU: Kondom
BABU: Kazi yake nini?
MJUKUU: He babu hujui kazi ya hiyo?
BABU: Sijui nambie
MJUKUU: Duh, mie huwa natumia kwa kuivalisha sigara wakati wa mvua ili niweze kuvuta bila sigara kulowa
BABU: Aise wazo zuri sana...........Babu akaenda dukani
BABU: Aise hebu nipe kondom tatu saiz ya sigara Spoti

UNAKOSEA KUMEZA

MGONJWA: Dokta zile dawa za rangi mbili ulizonipa hazini saidii kabisaa
DOKTA: Inawezekana unakosea wakati wa kumeza, kwa vile vidonge vya kijani na nyeupe, wakati wa kumeza unatanguliza ule upande wa kijani kwanza, na kwa vile vyekundu na njano, uwe unameza ukitanguliza upande wa njano kwanza halafu nipe matokeo baada ya siku 5.

ULEVI NOOOOMA

Baada ya ulevi wa hali ya juu jamaa kaamka asubuhi kakuta kumbe alibeba changu, 
CHANGU: He jamani tulishughulika bila kondom
JAMAA: Pombe mbaya sana tulijisahau
CHANGU: Usije ukawa na UKIMWI jamani
JAMAA: Ahh wapi nimepima wiki iliyopita nilikuwa fresh
CHANGU: Dah afadhali, maana sina mpango kabisaa wa kuambukizwa tena

5 December 2012

KILA KAZI NI MUHIMU

MWALIMU: haya watoto leo kila mtu atuambie kazi anayofanya mzazi wake, haya wewe?
MTOTO 1: baba yangu injinia
MWALIMU: Safi na wewe
MTOTO 2: Mama yangu nesi
MWALIMU: Safiii, wewe
MTOTO 3: Mama yangu changudoa
MWALIMU: Pumbafu mkubwa wewe, kwanini unamdhalilisha mama yako, haya nenda mwenyewe kwa mwalimu wa nidhamu mwambie kwanini nimekufukuza...........baada ya dakika kumi mtoto karudi
MWALIMU: Umemwambia?
MTOTO 3: Nimemwambia, kasema kila kazi ni muhimu wake, kaniomba na namba ya simu ya mama yangu

DAH NETWEK IMEKATA

Ngriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
MJAMAA: Halloooooooooooooo
MDADA: Mambo swity
MJAMAA: Poa vipi umenimiss?
MDADA: Ile mbaya si ndio maana nimekupigia
MJAMAA: Nambie
MDADA: Honey naomba laki mbili na nusu nianze kutayarisha vitu vya Krismas
MJAMAA; Haloo, haloo, haloo, he tigo nao wameshakorofisha network, halooooooooo dah wala hatusikilizani

VIFAA VYA KUTEMBELEA

TAA NA SAA3 December 2012

HAKUNA SIRI YA WATU WAWILI

Hahahahahaha wahenga walisema hakuna siri ya watu wawili, sasa hahahahaha sasa uwiiiii we umeshawahi kuwa na wapenzi zaidi ya wawili, kwa misingi hiyo ni kuwa wewe huna sehemu za siri hahahahahahaha. NA KWA WALE AMBAO WANA WAPENZI ZAIDI YA KUMI UNATOFAUTI GANI NA CHIZI ANAETEMBEA UCHI BARABARANI, KILA MTU KISHA MUONA WALA HAKUNA ANAEMUANGALIA MARA MBILI HAHAHAHAHAH, USHAURI HUNA HAJA YA KUFICHA CHOCHOTE WE TUPA NGO KULEEE SEPA HAHAHAHAHAHAH

KUJUA KUSOMA USUMBUFU


Dah kumbe kujua kusoma sio lazima faida. Tena mara nyingine ni hasara. We fikiria uko katikati ya mji, unataka kujisaidia, hakuna choo cha umma, unaona kakichochoro fulani uawahi unataka kujisaidi unakuta maandishi makubwa, USIKOJOE HAPA. Unakuwa mdogooo, ungekuwa huji kusoma wala isingekusumbua,ungemaliza shughuli yako na kutoka mwepesiiii. Una shida na mtu, unamfuata kazini kwake unakuta kibao kimeandikwa usiingie hapa, unabaki umezubaa nje unasubiri namna ya kuomba ruksa uingie, ungekuwa hujui kusoma ungeingia na kumaliza ishu zako na kusepa. Sababu tummejua kusoma, vibao hivi vya usikae hapa, usipite hapo, hakuna kazi, mbwa mkali, nyumba hii inalindwa na umeme, vinatufanya tuwe waoga hata kama hakuna kitu. Iko haja ya kuanzisha shule ya kufuta kujua kusoma na kuandika. Hii mifesbuk wala isingekuwa ishu

ALAAA KUMBE NDIO MAANA WADADA HAWAWAGI MAFUNDI MAGARI

KUMBE NDIO MAANA WADADA HAWAWAGI MAFUNDI MAGARI, AHAAAAAAAA SASA NIMEJUA

UKIKOHOA TU UMEHARISHA OHOOO

Jamaa aliajiriwa kwenye famasi, tatizo lake alikuwa msahaulifu sana, kila mteja akija kutafuta dawa, anajikuta kasahau imewekwa wapi, ikawa kazi yake iko hatarini. Siku moja kaja mteja anakohoa, akatafuta dawa ya kikohozi hakuipata akachukua dawa ya kufungua tumbo akamkabidhi mgonjwa tena akamwambia anywe pale pale chupa nzima kisha akamruhusu aende, mgonjwa hakwenda mbali, katembea kidogo kisha akaegemea nguzo ya umeme. Muda mchache baadae bosi wake akamuuliza kama ameuza chochote;
JAMAA: Ndio kuna mteja alikuja anakohoa nikatafuta dawa ya kikohozi sikuipata nimemuuzia dawa ya kufungua tumbo.
BOSI: Hiyo dawa kamwe haiponyeshi kifua
JAMAA: Najua haiponyeshi lakini inazuia, si unaona mgonjwa yule pale kaegamia nguzo, toka kanywa dawa anaogopa kukohoa

1 December 2012

BABA HIZO ZA NINI?

1st December-siku ya ukimwi duniani-
Mzee anaejiita wa kisasa alienda na mwanae famasi kununua kondom. Alipoulizia akajibiwa ziko za viboksi vyenye kondom  tatutau, sitasita na zilizo fungwa 12 kwa paketi;
DOGO: Baba hizo za nini?
BABA: Hizi zinaitwa kondom, huzuia maambukizi ya UKIMWI wakati wa kujamiiana.
DOGO: Kweli hata sisi tulifundishwa shuleni, sasa mbona zinafungwa kwa paketi tofauti?
BABA: Hizo zilizofungwa 3, kwa ajili ya vijana wanaopenda kwenda klabu wikiendi. Moja ya Ijumaa, nyingine Jumamosi na ya tatu Jumapili. Zile sitasita ni kwa ajili ya wale wenye nyumba ndogo, mbili Ijumaa, mbili Jumamosi mbila Jumapili. Hizi za kumi na mbili ni za walio katika ndoa, ya kwanza Januari, ya pili Februari hivyohivyo mpaka mwaka unaisha.

KIJANA WANGU HASUMBUI KABISAAA KITABIA

DEVI: Nina bahati sana, nina kijana wangu kwa kweli hanisumbui kabisa kitabia
JUMA: Anavuta fegi
DEVI: Hajawahi kuonja
JUMA: Pombe?
DEVI: Hajawahi kuonja
JUMA: Madem
DEVI: Hana habari kabisaa
JUMA: Dah bangi? madisco?
DEVI: Hashughuliki kabisaaa
JUMA: Ana umri gani?
DEVI: Mwezi ujao anatimiza miezi 6