HATUPIMI BANDO

10 November 2012

ZIMEBAKI SIKU KUMI TU

Mzee karudi kwa mkewe akitoka hospitali akiwa na sura ya huzuni sana;
MKE: Nini tena
MUME: Daktari kanambia ugonjwa nilio nao italazimika niwe nakunywa kidonge kimoja cha dawa kila siku kwa maisha yangu yote.
MKE: Sasa ndio uwe mnyonge hivyo? Mbona watu wengi duniani humeza vidonge kwa mtindo huo
MUME: Tatizo lake kanipa vidonge kumi tu, si ina maana maisha yangu bado siku kumi tu zimebaki

No comments: