PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

WATOTO WALE NI WANANI?

 
Kasheshe ni pale unapompa  binti mzuri mjamzito lifti kwenye gari lako, halafu anazimia. Kasheshe zaidi ni pale baada ya kumkimbiza hospitali, anapewa matibabu na kujifungua na kudai aliyemleta hospital ndie mwenye mimba. Ubishi mkali unazuka, na binti anang’ang’ania wewe ndie mzazi mwenzie. Unakuja juu na kuomba vipimo vifanywe ukweli ujulikane., kasheshe linaongezeka utamu pale inapogundulika kuwa, si tu kwamba wewe si baba wa mtoto yule bali huna uwezo kabisa wa kuwa baba. Hapo ndipo kasheshe linafikia upeo wa juu kwani unaanza kujiuliza wale watoto watatu ulionao nyumbani ni wa nani?

Comments