HATUPIMI BANDO

16 November 2012

TUUNGE MKONO HUDUMA MBOVU


Nimewashtukia, nawaambia nimewashtukia ohooooo, tutaonana wabaya hayaaa. Kila mtu anajua waBongo huwaga hawana noma wala nini kuhusu ubora, wanachojali ni kuwa kitu kimewezekana, sasa hizi ishu mnazotaka kuanzisha sasa mi nadhani ni njama zenu za kawaida za ufisadi tu unaonaee, eti ohh kuanzia sasa mtu ukiwa na lain yako unaweza ukahamia mtandao mwingine ukiona ule wa zamani unazingua, sasa hayo ndio maneno gani, halafu kwanini mmeona nimejikwaa kidogo ndio eti siku hiyohiyo ndo mnaanza kupigia debe hiyo ishu? Mi nawashauri wa Wabongo wenzangu jamani tusikubali kuburuzwa, hawa mafisadi tukiwaachia kesho watatoa amri eti kwenye daladala lazima kuwe na AC, na hakuna ruksa watu kusimama, yaani hii itakuwa dizasta kwenye biznes si mnaonaee, wote  sie ni wabongo tunajijua haya mambo madogo madogo huwa wala hatumaind sasa jamaa wanaanza mbali eti ooh namba moja unaweza ukahama mtandao. Kesho wenye daladala mbovu wote na mitandao mibovu, vyama vya siasa vibovu, hoteli mbovu, gest mbovu, tukutane jangwani kudai haki ya kuwa na huduma feki, mbona simu feki ruksa? Tena eti kusudi wananchi wasipate gharama si mnaonaee

No comments: