PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

TUKOJOE KIDOGO

Jamaa alikuwa anakojoa kitandani kila siku akaona heri aende hospitali kumuona daktari;
DAKTARI; Ukiwa umelala huwa unaota ndoto?
JAMAA: Ni kweli dokta huwa naota kashetani fulani, huwa kanakuja kananiambia ,'Tukojoe kidogo', basi mie hulazimika kukojoa nako
DAKTARI: Basi ukilala kakija tena kakikwambia hivyo , we kaambie tumeshakojoa sawa. Nenda urudi kesho tujue maendeleo,,,,,,,,,,kesho yake jamaa akarudi kwa daktari;
DAKTARI: haya vipi umeamkaje leo lile tatizo limeacha?
JAMAA: Leo ndio imekuwa mbaya zaidi. Kale kashetani si kamekuja kakanambia tena, 'Tukojoe kidogo', Nikakajibu kama ulivyoniambia, nikasema,'Tumeshakojoa", kakasema 'Basi tunye kidogo'

Comments