PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NAITWA MMEWANGU

Jamaa mgeni kabisa kaajiriwa kwenye kampuni;
SUPAVAIZA: Mheshimiwa unaitwa nani?
JAMAA: Naitwa John.
SUPAVAIZA: John nani? Unajua jambo ambalo nimeligundua ni kuwa watu mkianza kuitana majina ya kwanza mnazoeana na kazi inakuwa haiendi. Mi sio rafiki yako mi ni Supavaiza wako, kwa hiyo tafadhali nambie jina lako kamili
JAMAA: Naitwa John Mmewangu.
SUPAVAIZA: Haya Bwana John endelea na kazi

Comments