PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

MAJINI YAPEWE USAFIRI SASA


Kwa kweli hili jambo nadhani ni muhimu sasa lichukuliwe hatua za dhati, na kikubwa nashukuru kuwa limeanza kuongelewa. Tangu ningali mdogo, usafiri wa majini umekuwa unapuuzwa kabisa, nashangaa sijawahi kusikia Wabunge wetu wakitetea au kutoa ushauri kwa jambo hili ambalo ni mojawapo ya kero kubwa. Kitu ambacho kinaonyesha dharau kwa wahusika. Nakumbuka katika miaka yangu yote ya maisha nimekuwa nikionyeshwa wazee ambao wanafuga majini, na hata kuelezwa hadithi nyingi za majini. Pia nimesha sikia watu waliokumbwa na majini, watu waliotupiwa majini na kadhalika. Nimeshasikia kuna majini wa aina mbalimbali, jini mahaba ni moja ambalo liko maarufu sana, labda sababu nasikia walionalo wanafaidi sana mambo fulani. Nilisoma katika vitabu vya Alfulela Ulela majini mbalimbali, likiwemo Jini Kashkash, lakini ni mara ya kwanza kusikia nia ya kubainisha kinachokwamisha usafiri wao. Hongera sana kwa hili hasa ukichukulia kumekuwa na maendeleo makubwa ya barabara za binadamu nchini kote. Nategemea baada ya miaka michache majini watakuwa na treni yao bora isiyo na msongamano, daladala zao na kadhalika ili nao wasafiri bila kero ambayo lazima katika mabainisho hilo litaonekana.

Comments