PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

MABOYFRIEND TANZANIA KUGOMA MIEZI 2

-->
Chama cha Maboifrend Tanzania (CHACHAMATA) katika mkutano wake mkuu wa 2012 kimeamua kufanya mgomo utakaoanza kesho tarehe 1.12.2012 na kuisha 16.2.2013. Nia na madhumuni ya mgomo huu ni kupinga  vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia wanavyofanyiwa wanachama wake kwa kulazimishwa mambo ambayo kimsingi hayana uhusiano wowote na mapenzi.
Imekuwa ni kawaida mageloflend wengi kudai  vitu kama kununuliwa simu za bei inayozidi hata mshahara wa boifrend wao, kisha baada ya hapo kudai kununuliwa muda wa maongezi kwa haohao maboifrend, jambo ambalo linawaweka maboifrend katika wakati mgumu wa kuhangaikia kutafuta pesa za simu tu. Kuna wageloflend wengine hudai kupewa magari, na baada ya hapo kutegemea  fedha ya petroli na matengenezo kutoka kwa waliowanunulia, hii inatatizo kwani fedha nyingi za maendeleo ya wananchi zinabadilishwa matumizi na kuwa matumizi ya hawa wageloflend. Kuna maboifrend waliolalamika kuwa wanadaiwa matumizi lakini hawaruhusiwi kwenda kazini sasa hii ni wazi ni tatizo. Tuna lipoti ya maboyfrend ambao wakati huu wako lumande, wengine wamefungwa na wengine wameishiwa hawana hata hela ya kula kutokana na kulazimishwa kutoa chochote ili penzi liendelee.  Na ukiangalia yote haya hayana uhusiano wowote na mapenzi. Katika mkutano huu tunaiomba selikali wakati boiflend anakuwa kizimbani kwa kukwapua hela na aliyefaidika na ukwapuzi huo nae awe mshtakiwa mwenza. Hivyo basi chama kimewaagiza makatibu wa vyama kuanzia vitongojini kuelekeza wananchama wao wasitoe zawadi yoyote kwa mageloflendi wao mpaka siku mbili baada ya ile sikukuu ya KITAPELI ya Valentine. Tunategemea kupata feed back toka kwa viongozi wa ngazi za chini kuhusu utekelezaji wa hili. ONYO KWA WALE WATAKAOKIUKA, CHAMA KITAFANYA KILA MBINU MUWAOE HAO MLIOWAPA ZAWADI   hii itahakikisha unapata kifungo cha kuwa na huyohuyo mmoja maisha yote, au kumchonganisha na mkeo tuone moto unapowaka.
 PREZIDA
CHACHAMATA

Comments