PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

HATA MIMI SIJUI JIBU

Juzi kwenye hivi vipindi vya TV ambavyo wadada wameshika hatamu kutangaza, na huwa wanawauliza watu mambo mengi tu nilisikia kali. Mdada alikuwa kamkaribisha daktari wa hospitali wa wagonjwa wa akili, ambaye alielezea kuwa mtu anaweza akaonekana mzima kabisa , lakini ukimuuliza maswali fulani rahisi ukaweza kujua kuwa mtu huyo ana matatizo ya akili;
MDADA: Daktari unaweza kutufahamisha ni maswali aina gani?
DAKTARI: Kwa mfano naweza kumuuliza mgonjwa swali la kihistoria kwa mfano nikasema,'Dr Livingstone alifanya safari tatu kwenda Ujiji na ndipo kifo kikamkuta, sasa je nika katika safari ya ngapi alipofariki?'
MDADA: (kwanza alicheka kidogo) Watazamaji hayo ndio aina ya maswali  ya dokta, mi kwakweli sikuwa mzuri sana kwa historia wakati niko shule, sina jibu ila nategemea watazamaji kuna wengi mmekwishapata jibu....sasa dokta huwa hamna maswali rahisi yanayohusu jamii tuliyonayo leo? (....nikahamisha chaneli)

Comments