PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

HAKIMU KAIBIWA SAA YA DHAHABU

Baada ya kesi kufikia karibu na tamati, hakimu akawataka wazee wa baraza watoe ushauri;
HAKIMU; Wazee naomba mnipe ushauri kuhusu huyu mshtakiwa ili nitoe hukumu, lakini ningependa kuwashauri kuwa pamoja na kuwa maneno aliyosema polisi hayafanani na aliyoyasema mahakamani hilo lisiwe kikwazo. Kwa mfano wakati naingia hapa nilijikuta ghafla sina saa yangu ya dhahabu, nikawa nina uhakika nimeibiwa, lakini wakati kesi inaendelea nikakumbuka kumbe nimeiacha nyumbani kwenye drawer la nguo. Haya tuendelee....... Jioni hakimu akarudi nyumbani
MKE WA HAKIMU: Baba imekuwaje tena leo umetuma watu watatu kuja kufuata saa yako?
HAKIMU: Mi sijamtuma mtu yoyote
MKE WA HAKIMU: Haaa kaja mtu wa kwanza kasema umemtuma kuja kuchukua saa yako ya dhahabu tena kaelekeza kabisa kuwa iko ndani ya drawer mi nimempa, ila nikashangaa wakaja wengine wawili nikawambia mwenzao keshakuletea
HAKIMU: Loh mke wangu tumesha ibiwa

Comments