PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

BREAKING NEWWWWWWWWS--DOMOZEGE MIDDLE SCHOOL


Katika jamii ya binadamu wa Bongo kuna hawa wanaoitwa ‘DOMO ZEGE’.  Kutokana na ubaguzi wa hali ya juu wa kijinsia  jina hili linahusu wanaume tu. Wamama wenye tatizo hili husifiwa kwa kuwa na staha!!!!!!!!. DOMOZEGE ni mkaka ambae anaweza kumuona mdada anaempenda lakini kila akikutana nae mdomo unakuwa mzito  kujieleza ishu yake, kinyume cha jina lenyewe DOMOZEGE si kwamba hawawezi kuongea, aa wapi wanawezakuwa waongeaji saaaana lakini ikifikia kueleza hisia zao kuhusu mdada wanaempenda akili ina siz. Si mara moja domo zege hunyang’anywa tonge mdomoni. Cha ajabu wakishanyang’anywa eti ndio wanaanza kufunguka,’Ohh unajua anti mi nilikuwa na mipango mingi sana na wewe sasa naona bradha kaniwahi’, na mara nyingi hujibiwa,’Jamani kwanini hukusema?” Kutokana na tatizo hili kuwa kubwa, maana kipimo cha ukubwa kinakuja kutokana MADOMOZEGE siku hizi wamechukua staili ambayo inaleta fujo kwenye fani, wameanza kumwaga zawadi za bei mbaya. Utakuta DOMOZEGE anatoa iPhone5 mtaa huu, mtaa mwingine BB, kule chini anamwaga minoti tu eti ndio iongee kwa niaba yake, au siku hizi kuna staili ya kununulia watu Verosa, sasa huu ni ukorofi katika fani. Shule maalumu kwa ajili ya MADOMOZEGE zinaanzishwa ili kuwa saidia wenzetu hawa, na kutokana na maendeleo kutakuwa pia na masomo kwa ajili ya akina mama ambao wanaona nao UDOMOZEGE unawakwaza. UMEONAEE

Comments