PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

AFANDE NIMEBAMBIKIWA KESI

Jamaa kasimamishwa na trafiki kwa kosa la mwendo mkali;
TRAFIKI: Mheshimiwa unajua ulikuwa unakimbia spidi kali sana?
DREVA: Sasa leseni sina, gari niliiba, halafu chini ya kiti nina pisto ya wizi unadhani ntaendesha polepole
TRAFIKI: Mungu wangu kumbe we jambazi?
DREVA: Si jambazi tu, pia huwa nauza viungo vya binadamu, kwenye buti kuna vipande vya miili vya watu....trafiki haraka akaita msaada wa polisi wenzie waliofika baada ya muda mchache wakiogozwa na afande mkubwa
AFANDE: Askari vipi tena hapa?
TRAFIKI: Afande nimelikamata jambazi sugu. Halina leseni, gari ni la wizi, limeficha pisto chini ya kiti na kwenye buti kuna vipande vya miili ya binadamu.
AFANDE: Leseni yako iwapi?
DREVA : Hii hapa afande na kadi ya gari hii hapa
AFANDE: Askari mbona leseni iko safi, na gari lake sio la wizi, hebu sachini gari kama kuna hivyo vitu alivyoviona askari....gari likasachiwa lilikuwa safi
DEREVA: Afande askari kaninyanyasa sana huyu kasema yote hayo asiponibambika atasema nilikuwa naenda mwendo kasi
AFANDE: Mheshimiwa wewe nenda, jeshi litajua namna ya kushughulika na huyu askari aliyekusumbua

Comments