HATUPIMI BANDO

7 October 2012

SIKUZANI MUMEO ANAKUHITAJI

Binti wa Kizaramo Bi Sikuzani aliolewa na na Chacha, Mkuria safi wakawa wanaishi Musoma kwa mapenzi ya hali ya juu. Siku moja wakaamua kuja Kisarawe kuwasalimu wazazi wa Sikuzani. Bahati mbaya Chacha akaugua malaria kali sana na kwa siku mbili hakuweza kula. Hatimae siku ya tatu mama mkwe aliingia kwenye chumba cha mkwewe kumjulia hali akamkuta kidogo ana nafuu;
MAMA MKWE: Vipi baba unadhani tukuletee nini?
CHACHA: Mukiniretea uchi wa moto nitacharibu kidogo
MAMA MKWE: (Aliondoka kwa aibu) We Sikuzani, mumeo naona amepona anakuhitaji upesi 

No comments: