HATUPIMI BANDO

6 October 2012

KWA MBAAALI NILIANZA KUONA


Mkutano wa mwaka wa dunia wa akina mama walioolewa ulikuwa inaendelea, na akina mama kutoka nchi mbali mbali walikuwa wanatoa ripoti ya utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa mwaka uliopita;
MAMA UK: Baada ya maazimio ya mkutano wa mwisho kuwa lazima waume zetu waanze kupika chakula wenyewe, nilipofika London nilimueleza mume wangu. Siku ya kwanza sikuona kitu, siku ya pili pia sikuona kitu, siku ya tatu mwenyewe aliingia jikoni na kuanza kupika (Makofi na vigelegele)
MAMA USA: Baada ya maazimio ya mwaka jana niliporudi Washington, nilimwambia mume wangu kuwa sitampikia wala kumfulia tena. Siku ya kwanza sikuona kitu, siku ya pili alifua nguo chache, siku ya tatu mwenyewe alifua na kupika (Makofi vifijo na vigelegele)
MAMA TZ: Baada ya maazimio ya mwaka jana, niliporudi kwetu Musoma, nikamwambia mume wangu kuanzia leo, lazima ujipikie mwenyewe, ufue nguo zako mwenyewe, ufagie nyumba na kutandika kitanda mwenyewe. Siku ya kwanza sikuona kitu, siku ya pili sikuona kitu, siku ya tatu sikuona kitu, siku ya nne kwa mbali nilianza kuona kwa jicho la kushoto, maana uvimbe usoni ulianza kupungua  


No comments: