PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

KAMA WATANGAZAJI WETU WA VIPINDI VYA MIPASHO WANGEKUWA MARAIS

Hivi hawa wadada wenye mipasho wanaotangaza kwenye redio zetu kwa mfano kila mmoja angechaguliwa kuwa rais wa nchi mbalimbali, vita zingeisha mara moja. Lakini utamu ungekuwa kwenye hotuba za kila mwezi za marais.
1. (Rais wa TZ) Shostiii haloooooo, nisikilize vema dada, mtu mwenyewe kilemba kama umebeba mtungi wa pombe ya kienyeji, hebu achia ziwa langu babu, kila asubuhi watu hatulali eti unataka kubadili mpaka, kama unapenda sana mipaka si ufuge nyau. Basi kwa taarifa yako babu ole wako utie mguu kwenye maji hayo. Ndo utajua kinyago cha mpapure ni nini halooooooooo
2. (Urais wa Marekani) Shosti nani kakudanganya kuwa na wewe unafaa kuwa rais, huo mkorogo wa kuchanganyiwa na Wakongo, basi unajiooona mweupeee. Basi mie ngozi yangu orijino bibie. na nawashauri wananchi wachague kitu orijino, rais gani hata ngozi tu ya Mchina, haloooooooooo chezea ngozi nyeusi weye, hapa Jaluo orijino na uchaguzi pia nashinda
3. (Uingereza) Jamanieeeeeee humu ndani sasa ishakuwa shida, imefika muda kieleweke, wanaume wawe wanaume wanawake wawe wanawake, sio dume zima unapaka wanja halafu unajitie eti nawe mwenzetu  akuuu, polisi wakamateni wote hao wanaojifanya wadada wakati wenyewe wakaka, mwanamke gani guu limekakamaa utadhani nguzo za Tanesco za Tanzania.

Comments