HATUPIMI BANDO

23 October 2012

BREAKING NEWSSSSS. KUMBE TANZANIA NI MUUNGANO WA TANGANYIKA NA VISIWA VYA ZIMBABWE NA PEMBA

Kumbe muungano wa Tanzania ulifanyika mwaka 11964 kati ya visiwa vya Bahari ya Hindi vya Zimbabwe and Pemba na Tanganyika. Najua utabisha, mi shahidi yangu ni Mheshimiwa Philipo Augustino Mulugo -- Deputy Minister of Education and Vocational Training, na aliuambia ulimwengu wote kwenye presentation yake kuhusu 'Education for Employment, Developing Skills for Vocation' kwenye mkutano wa Innovation Africa Summit  uliofanyika tarehe 5th-7th October 2012, Westin Hotel, Cape Town, South Africa.

4 comments:

Anonymous said...

Ha haaa Anko, ya kweli haya? I didnt know, tena 11964..teh teh

John Kitime said...

YES LIVE BILA CHENGA HIYO

John Kitime said...

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philip Mulugo aliyejikanyaga na kusababisha gumzo kubwa Tanzania kuhusu namna alivyokuwa akiwasilisha mada kwamba Tanzania ni Muungano wa visiwa vya Pemba na Zimbabwe amejitetea na kusema aliteleza ulimi hivyo anaomba msamaha.

Anonymous said...

AIBU: Poor english skills, poor presentation skills, jamaa anasoma kila kitu yani yani hata information kuhusu elimu anaonekana hajui kama inavyotakiwa. Kikwete anipe mimi hiyo kazi tafanya vizuri kumliko