PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

BIA HOYEEEE

Kwanza naomba nitambue uwepo wenu wale watu wangu aka WABISHI DAMU unaonaee. Hawa watu wanaweza kununua ubishi, kubishana na redio, kubishana na magazeti, na kadhalika, kwa hiyo kabla ya kusema neno lazima utambue kwa heshima uwepo wao unaonaee. Uzuri wa watu hawa ni kuwa nchi yetu ina maendeleo makubwa kwa ajili yao, inalazimika sisi tusio wabishi kufanya kazi ya ziada ili japo kuwa wasiwe na ishu nyingi za kubisha unaonaee. Hawa watu wasingekuweko kama walimu wasingekuwa wanahamasisha wanafunzi kuwa na mijadala yenye mada kama zifuatazo;-
1. Baba na mama bora nani?
2. Jua na mvua bora nini? Unaonaee.  Mijadala kama hii ndio iliyoliingiza taifa letu katika janga la kuwa na wabishi hawa, ambao wengi siku hizi wanafanya shughuli za kugombania kushika nchi (....mmeshabisha dah...) unaonaee. Kwa kujua hilo ningependa kutangaza kuwa nimegundua kuwa vitu vingi hapa nchini vinaharibika kwa kutu, hebu fikiria mpaka vituo vya mabasi vinaanguka kwa kuliwa na kutu,madaraja, nondo, mageti, magari , vyote vinaharibiwa na kutu, na hata wabishi mtakubali maji ndio yanayoleta uharibifu huu mkubwa. Kwa kweli jibu ni wazi kabisa MAJI NI KITU CHA HATARI. Uliwahi kusikia bia imesababisha kutu? Au ukasikia oh kile kibanda cha kusubiria mabasi kimeanguka kwa kumwagikiwa na bia? Natangaza rasmi kampeni ya ACHANA NA MAJI KUNYWA BIA , MAJI YANALETA KUTU. Unaonaee  HAYA ANZENI KUBISHA KAMA KAWAIDA YENU

Comments