HATUPIMI BANDO

31 October 2012

Breaking newsss- Miss Legline yapata top 4

Baada ya mpambano mkali wa nani mwenye miguu bomba,kati ya washindani mia saba, wameweza kupatikana wanne ambao kuna utata kama wataweza kuwakilisha taifa wakashinda.

30 October 2012

TAREHE 21 JUNE 2012---Blog hii ilituma kichekesho chake cha kwanza,............

TAREHE 21 JUNE 2012---Blog hii ilituma kichekesho chake cha kwanza,............
DOKTA:        Umesema una ugonjwa wa kusahau sahau?
MGONJWA: Ndio
DOKTA:         Hebu nipe mfano wa kitu ulichowahi kusahau...
 na kuanzia hapo imekuwa taabu mjini. Juzi wadada wawili maarufu walikuwa na ugomvi mkubwa kutokana na mmoja kukataa kuntajia mwenzie jina kamili la blog hii, pia kuna habari kuwa washika dau watatu juzi waliachia dau na kugombania kusoma blog hii, bila kusahau wale jamaa zangu wa Zimbabwe ehh sorrryy ya samahani, Zanzibar narudia tena Zanzibar asante kwa simu mnazopiga wakati mko hapo sehemu mbele ya Hekalu la Ajabu mkiwa mnaendeleza utamaduni wa kupata urojo kila jioni endeleeni na simu senu zinaleta faraja. Waheshimiwa wa Italy aksante sana kwa kuwezesha hii blog kuwepo. Wazee wa Uingereza aksante sana kwa kuunga mkono, Swaiba Boston, aksante kwa encouragement. Ndugu na jamaa ambao huwa mnanipasia vibonzo kwenye simu, kupitia facebook, aksante sana, ntakapo chaguliwa kuwa Rais, muwahi kunikumbusha niwape ukuu wa Wilaya. Aksante sana Global Publishers, Millard Ayo, Spoti Starehe na wengi wengine ambao kwa namna moja au nyingine wameipiga jeki blog hii ili watu wengi zaidi waione. Sisi tunaendereaa japo tungefurahia kupewa matangazo, hatuwakasirikii waliotunyima matangazo kwa sababu zilizondani ya uwezo wao, kwa sababu kazi ya blog hii ni kuhakikisha kila mtu anacheka hata kama hutaki, nilicheka hata pale yule mdada wa kampuni kubwa aliponambia kampuni yao hailipiagi matangazo, teh teh teh teh kwa ukorofi naweka hilo tangazo la bure kwa wiki moja

BREAKING NEWSSSSSSS-KIBOKO YA WEZI WA MAGARI YAGUNDULIWA MWANANYAMALA

KUMEKUWEKO NA NJIA NYINGI TENA ZA GHARAMA ZA KULINDA MAGARI YASIIBIWE, NA SASA VIJANA WADOGO WENYE AKILI ZA KIDOT.COM WAMEGUNDUA NJIA MPYA YA KULINDA GARI. KAMA UNAVYOONA. MAKOFI KWA MAFUNDIIIII

MIKUBWA MIZIMA MNAOGOPA BUNDUKI YA KUCHEZEA

Majambazi yaliingia katika nyumba moja kuiba. Mwenye nyumba akaamka na kwa ujasiri mkubwa akachukua bunduki ya kuchezea ya mwanae na kuwatisha majambazi wenyewe wakawa wapole wakati mzee akaita polisi huku akiwalenga kwa ile pisto ambayo wao walidhani ni ya kweli. Wakati majambazi wamejikunyata wakiwa chini ya ulinzi wakisubiri polisi, mtoto wa mwenye nyumba akaamka;
DOGO: Nataka kwenda chooni
BABA: Nenda tu mi nimewakamata hawa wezi nangojea polisi waje
DOGO: Haoooo mikubwa mizima mnaogopa bunduki ya kuchezea

BIASHARA NGUMU, KITU KIPYA CHA APPLE

Mambo ni magumu hawa Samsung wanajidai wajanja sana sasa kwa mara ya kwanza epo wameamua kutoa kitu kipya.

29 October 2012

SHUGAMAMA NA KISERENGETI BOI CHAKE

Shugamami na Kiserengeti boi chake walifika guest moja kuomba chumba;
SHUGAMAMA: Naomba chumba, nipe dabo
MWENYEGESTI(Mlokole): Hapa hatuwapi chumba labda mngekuwa mke na mume katika ndoa halali
SHUGAMAMA:We baba we mbona una matusi? Huyu ni mwanangu
MWENYEGESTI: Samahani mama............Baada ya kupewa chumba mwenye gesti akamwita muhudumu,
MWENYEGESTI: Hebu kawachugulie wale maana yule mama amesema eti yule kijana ni mwanae............muhudumu akaenda kuchungulia kisha akarudi
MHUDUMU: Kweli ni mama yake, tena ana huruma sana, nimechungulia nimeona anamnyonyesha mtoto wake

Wapanya wa Ilinga tumechoka

Sisi wapanya wa Ilinga kwa kweli haki setu sina salauliwa sana. Selekali haitujali, mapaka yanaongeseka na hifyo sisi tunanyimwa haki setu sa msingi. Watu wanausa sumu sa kutuuliwa hasalani na selikali haichukui hatua sosote. Kwa hiyo SWELA nimeona mimi sina sida na guinchi gwenu nakwenda sangu, Muhungilage avanangu mbevali asandi sana
MWAMBEVA

PIGA MSWAKI UPATE BAHATI

Kila subuhi, amka na kitu cha kwanza anza kupiga mswaki meno yako. Hakuna kitu kinaudhi kama unaongea na mtu hajapiga mswaki, hata kama anakwambia jambo la maana unakuwa humsikilizi. Na kwa kweli waheshimiwa kwa wale ambao wana shida, usiende kuanza kueleza shida zako na mdomo unanuka , ujue hutasaidiwa. PIGA MSWAKI VIZURI

28 October 2012

ULE UGOMVI BADOOOOO HAUJAISHA

Kwa kweli hali bado ni ngumu, maana Mzee baada ya kuona kibano kina muandama, si kaamua sasa kumtia kabali ya miguu mama. Mpambano ni mkali jamani, kwani mama huyu si wa mchezo

BREAKING NEWSSSSSSSSSSSS KATA KEI YA KUFA MTU

Yaani mambo mengine tunapoiga basi yawe na mantiki sasa unaiga kitu  ambacho chanzo hujui. Na mbaya zaidi unapotaka kuiga wakati uwezo huna ohoooo

WAUZA KARANGA HUWA WANAENDA CHOONI?

Mara nyingine mtu ukikaa ufikirie kwa kina mambo fulani fulani unaweza ukashangaa  kuwa jambo linaloonekana ni la kawaida kumbe si kawaida kiviiile unaonaee. Wengi wetu ni wateja wazuri wa bar, wengine huingia bar kula nyama tu, wengine soda, wengine vinywaji vikali na kadhalika. Bar zetu zina utamaduni wa kuruhusu wafanyabiashara wengine wafanye biashara katika maeneo yao. Mi nataka tuwazungumzie hawa wauza karanga, tena wale wa karanga za kupima. Hebu tutafakari hivi katika zunguka zao bar moja kwenda nyingine si huwa wanapata hisia ya kuwa lazima wakajisaidie. Sasa swali wakati wanajisaidia zile karanga huziacha nje ya mlango wa choo au huingia nazo chooni? Na kama ni kujisaidia kichakani, si ndio mikono hiyo hiyo wanatumia kukupimia karanga? NAWAZA TU

27 October 2012

TOILET YA MUDA

Kutokana na ukata uliopo, tunaomba kwa kipindi kifupi wababa muwe mnatumia choo cha kulia, na wadada watatumia choo cha kushoto. Hii ni kwa muda tu, mara fedha za kutosha kujenga ukuta zitakapopatikana swala hili litarekibishwa. Aksante kwa ushirikiano wenu

NIPE NAMBA YAKE

MBONGO 1: Aise nina tatizo nipe ushauri. Kuna demu wangu nampenda sana lakini sio mwaminifu kabisa, hajui kukataa nifanye nini?
MBONGO 2: Nipe namba yake ili  nimkanye

KAMA WATANGAZAJI WETU WA VIPINDI VYA MIPASHO WANGEKUWA MARAIS

Hivi hawa wadada wenye mipasho wanaotangaza kwenye redio zetu kwa mfano kila mmoja angechaguliwa kuwa rais wa nchi mbalimbali, vita zingeisha mara moja. Lakini utamu ungekuwa kwenye hotuba za kila mwezi za marais.
1. (Rais wa TZ) Shostiii haloooooo, nisikilize vema dada, mtu mwenyewe kilemba kama umebeba mtungi wa pombe ya kienyeji, hebu achia ziwa langu babu, kila asubuhi watu hatulali eti unataka kubadili mpaka, kama unapenda sana mipaka si ufuge nyau. Basi kwa taarifa yako babu ole wako utie mguu kwenye maji hayo. Ndo utajua kinyago cha mpapure ni nini halooooooooo
2. (Urais wa Marekani) Shosti nani kakudanganya kuwa na wewe unafaa kuwa rais, huo mkorogo wa kuchanganyiwa na Wakongo, basi unajiooona mweupeee. Basi mie ngozi yangu orijino bibie. na nawashauri wananchi wachague kitu orijino, rais gani hata ngozi tu ya Mchina, haloooooooooo chezea ngozi nyeusi weye, hapa Jaluo orijino na uchaguzi pia nashinda
3. (Uingereza) Jamanieeeeeee humu ndani sasa ishakuwa shida, imefika muda kieleweke, wanaume wawe wanaume wanawake wawe wanawake, sio dume zima unapaka wanja halafu unajitie eti nawe mwenzetu  akuuu, polisi wakamateni wote hao wanaojifanya wadada wakati wenyewe wakaka, mwanamke gani guu limekakamaa utadhani nguzo za Tanesco za Tanzania.

KARIBU KWENYE KIKAO CHANGU CHA KWANZA


Ukiwa kama ndugu, jamaa na  rafiki  yangu, napenda kukukaribisha kwenye kikao changu cha kwanza kitakachofanyika nyumbani kwangu, maeneo ya Sinza kwa Mwaibula, tarehe 28/10/2012 mchana. Nahitaji mchango wako wa hali na mali kuniwezesha kununua gari, maana suala la usafiri hapa mjini limekuwa ni swala nyeti na lenye umuhimu mkubwa. Kufika kwako ndio mafanikio yangu karibu sana sana.. Ninaanza kupokea pledges mara moja, kutoa ni moyo si utajiri.

26 October 2012

DAH SIJUI NIMEINGIA MKENGE?

DAH SIJUI NIMEINGIA MKENGE? HALAFU NDIO WOTE WALE WENGINE BASI TENA?

VIATU VYA RANGI MBILI

Mpolisi kafika kituoni amevaa viatu vya rangi tofauti, kimoja cheusi kingine cheupe.
Afande; Askari kwanini umevaa viatu rangi tofauti? Nyie ndio mnatia aibu jeshi, rudi nyumbani kavae vizuri. Baada ya muda mpolisi akarudi amevaa vile vile.
Afande: Askari mbona umerudi vilevile ?
Mpolisi: Afande nimefika nyumbani nikakuta hata vile vya nyumbani kimoja cheusi kingine cheupe.

KUJITUMA MUHIMU LAKINI UKUMBINI??????


25 October 2012

NANI KAMFUMANIA NANI?

Mmama alikuwa kapanga na Mchuchu wake waende guest-house fulani wakavunje miiko ya ndoa. Ile anafika reception akakutana na mumewe akitoka na mdada;
MMAMA: Nimekukamata tena uzuri wake nimekuja na shahidi kabisa.....Mume bila kupaniki akamgeukia yule mdada;
MUME: Mama ushauri unaona niliyokwambia, tungewahi kutoka tungewakosa, umeona kusubiri ilivyosaidia. Kesho tunapokuja kwenye kesi ofisini kwako ushahidi mwenyewe unao

MAMAA MTOTO WAKO SIO MALAIKA

Familia yenye mkwanja kidogo, walikuwa wanaishi katika kabangaloo kao kenye ghorofa moja. Mamaa alikuwa kajifungua mtoto wa pili ana wiki mbili tu
DOGO: Mamaaaaaaaaaa njooooo huku chumbani kwakooo
MAMA: Kuna nini?
DOGO: Njooooo mama
MAMA: Heee wee mtoto yuko wapi?
DOGO: We ndio umenidanganya, ulisema mtoto wako malaika, nimemtupa nje kashindwa kupaa

23 October 2012

KANIDHURUMU VOGUE NILILOIBA

Siku mbili baada ya kuachiwa huru na mahakama kwa kuonekana hana kosa kwa wizi wa Vogue la pedeshee mmoja, jamaa alikuwa mahakamani tena safari hii kwa hakimu yule yule  akiwa amemshtaki mganga wake wa kienyeji kwa utapeli;
HAKIMU: Nini tena bwana naona umerudi sasa kama mlalamikaji kuna nini?
JAMAA: Mheshimiwa si unakumbuka juzi umeniachia huru kwa kutokuona nina hatia ya kuiba vogue? Basi huyu mganga alinipa dawa nishinde ile kesi, sasa alipoona namwambia kwa sasa sina hela ya kumlipa kwa kazi yake kaamua kunidhurumu Vogue nililoiba.

BREAKING NEWSSSSS. KUMBE TANZANIA NI MUUNGANO WA TANGANYIKA NA VISIWA VYA ZIMBABWE NA PEMBA

Kumbe muungano wa Tanzania ulifanyika mwaka 11964 kati ya visiwa vya Bahari ya Hindi vya Zimbabwe and Pemba na Tanganyika. Najua utabisha, mi shahidi yangu ni Mheshimiwa Philipo Augustino Mulugo -- Deputy Minister of Education and Vocational Training, na aliuambia ulimwengu wote kwenye presentation yake kuhusu 'Education for Employment, Developing Skills for Vocation' kwenye mkutano wa Innovation Africa Summit  uliofanyika tarehe 5th-7th October 2012, Westin Hotel, Cape Town, South Africa.

22 October 2012

HEBU FYATUA

TATIZO LA NYIE ASKARI HUWA MNASAHAU KUWEKA RISASI, MBONA SIIONI? HEBU FYATUA NIONE KAMA IMO

INGLISH IZ IZZY LANGWEJ


Hawa Waingeleza wanazingua sana, kwa hiyo na mimi naona nianzishe uamsho wangu ili wasituzingue tena. Kiukweli Kiingera ni rahisi sana sasa, ila hawa jamaa wakishirikiana na serikali dhalimu za Marekani na Uingereza wanakifanya kigumu makusudi ili watuchanganye sisi huku Afrika. Kwa hiyo basi kwa kutumia nguvu za uamsho natoa maelekezo machache munielewe na kisha wote tushirikiane kuondoa ukiritimba wa kimangimeza unaotawala katika hili.
Hebu fikiria kwanini kitu kitamkwe Hea, lakini kiandikwe hair? We fikiria kitu kidogo tu kinatamkwa mai eti kinaandikwa my, si mbinu tu za kuchanganya watu. Kwa hiyo naanza kwa kuchoma matairi hapa mtaani ili kuanzia kesho watu wote wafuate uamsho huu.
Mosquito…iandikwe moskwito
House - haus
Teacher - ticha
Chairman - cheamen
Facebook - fesbuk
Like -laik
Poke –pok
Najua kuna mengi yanawaudhi naomba wafuasi wangu mbadilke hata nikitekwa msikubali
Kwanini tusiandike aifon badala ya neno gumu iphone?
Eti Blackberry hwai? Ni rahisi tu blekberi. Tusaidiane uamsho sambaza kipeperushi hiki. Utakuta baada ya muda mfupi kila mtu ataweza kuandika kiingereza. Biliv mi it iz veri izzy,tu rait inglish langwej

ANTI MALARIA CAMPAIGN


21 October 2012

KAOGEEEEEEEEEEEEE


NGOJA ARUDI AFANDE

Jumamosi moja Trafiki kamkamata jamaa aliyekuwa anaendesha gari spidi, kila jamaa alipojaribu kujitetea Trafiki hakusikiliza, akamwambia mhalifu , 'Kwanza twende kituoni sitaki kusikia chochote'. Walipofika kituoni askari aliendelea na shughuli zake akatokea baada ya masaa mawili na kumweleza mhalifu, 'Nyie madereva wakorofi sana, nikikuachia utadai eti nimechukua rushwa, kwa hiyo kesi yako italazimu tumsubiri Mkuu wa Kituo kaenda kwenye harusi ya binti yake akitoka huko na furaha zake labda atakuachia'. Mhalifu akajibu kwa upole, 'Afande sidhani kama atarudi na furaha maana mie ndie Bwana Harusi, hivi nilikuwa nakimbilia kanisani niwahi kuoa".

20 October 2012

PIGA HONI KAMA UNAIPENDA YANGA

Jamaa kafika kwenye trafic lights nyekundu, mbele yake kuna gari akasimama kusubiri taa zibadilike rangi. Akaona kwenye gari lililo mbele yake stika imeandikwa 'Kama unaipenda Yanga piga honi'. Jamaa kwa kuwa alikuwa mpenzi wa Yanga akapiga honi. Si  dreva wa gari lenye stika akashuka kwenye gari yake na kumfuata jamaa. 'We mpumbavu nini? Si unaona taa bado nyekundu unapigapiga honi unataka niingie barabarani kwa ajili ya haraka zako, acha hizo utalambwa makofi ya kelbu wewe?'

NIMESHAVAA KONDOMU

Mateja wawili walikuwa wanajitayarisha kujidunga sindano za madawa ya kulevya;
TEJA 1: Sasa unajua siku hizi kuna Ukimwi wanasema tusitumie sindano moja watu wawili
TEJA 2: Unaniona mi fala sioo? Mwenzio nimeshavaa kondomu we jidunge halafu nipe na mie

MY SHOES CLARKS


MTAJIJUU ROAD


NYIE NATAKA KUFUNGUA BENKI

Jamaa kaingia benki;
JAMAA: Nyie wapumbavu nataka kufungua akaunti
BANKER: Mzee mbona matusi ongea tu utasaidiwa
JAMAA:Hebu acha ujinga nifungulie akaunti
BANKER: Mzee tunadhani we uende benki nyingine umeshatukosea adabu vya kutosha
JAMAA: Mjinga mkubwa  hebu muite meneja wako pambaf.
Banker akamuita meneja;
BANKER: Huyu jamaa toka ameingia ni matusi tu nimemuomba aende benki nyingine
MENEJA: Tukusaidiaje mzee?
JAMAA: Sikiliza nimeshinda bahati nasibu hapa nina milioni 150, hawa wapumbafu hawataki kunifungulia akaunti
MENEJA: Nyie wapumbavu wakubwa hebu mfungulieni huyu mzee akaunti upeshi, shenzi nyie.

MIE ATAUTAMBUA MWANDIKO WANGU

FARIDA; Baby wangu kaniudhi hebu nipe simu yako nimtukane
RITHA: Kwani kutumia simu yako?
FARIDA : Hawezi kupokea akiona namba yangu, au ngoja nimtumie txt nimchambeee
RITHA: Haya chukua
FARIDA: Hapana andika wewe, mimi nikiandika atautambua muandiko wangu

18 October 2012

BABA YANGU HAFANYAGI KAZI

Nimetembelea nursery school leo, nikapewa nafasi ya kuongea na watoto ambao kama kawaida yao wana akili kuliko tunavyofikiria;
MIMI: Haya nani anajua kazi ya baba yake?......Watoto wakanyanyua mikono juu wote, nikamchagua wa kwanza;
MIMI: Ehee baba yako anafanya kazi gani?
MTOTO: Baba yangu mjenzi anajenga magorofa
MIMI: Sawa na wewe
MTOTO 2: Baba yangu dokta anachoma watu sindano
MIMI: Sawa na wewe
MTOTO 3: Baba yangu dreva anaendesha magari
MIMI: Na wewe hapo katikati baba yako anafanya kazi gani?
MTOTO 4: Baba yangu hafanyagi kazi, yeye mwanasiasa
MIMI: Duh haya watoto wazuriiii 

SIMBA YUPO?

Simu ililia saa nane ya usiku mume akapokea, kisha akaikata kwa hasira baada ya kusikiliza kwa muda;
MKE: Nani tena saa hizi?
MUME: Naona ni mmoja wa hawa wapenzi wa mpira, mjinga sana anauliza Simba yupo? Si akaulize kwa Rage

YAANI CHA KUSEMA HAKUNA


BABUUUUUU


HAKUNA CHA BABU WALA NINI!!!!!!!!!!!!!!!!

MKE WANGU HEBU NAMBIE UKWELI

MUME: Mke wangu, niwe mkweli pamoja na kuwa kwa sasa tuna watoto sita mimi bado nakupenda sana. Na hakuna kitu kitakachoweza kunifanya niache kukupenda, I love you honey. Nina swali moja tu, huyu mtoto wa nne mbona yuko tofauti na hawa wenzie sita, mkorofi, hataki shule yaani tabu tupu? Mke wangu nambie tu kama ana baba tofauti na wenzie, kiukweli halitabadili mapenzi yangu kwako.
MKE:(Huku akipiga magoti) Mume wangu najisikia vibaya naomba unisamehe ni kweli huyo mtoto baba yake ni tofauti na wenzie
MUME: (Machozi yakimlengalenga) Dah mke wangu... baba yake ni nani?
MKE: Baba yake ni wewe.

17 October 2012

YAANI LEO NDIO NIMEPATA JIBU...

Jamaa alivunjika mguu akaepelekwa hospitali;
DAKTARI: Imekuwaje mpaka ukavunjika mguu?
JAMAA: Miaka kumi iliyopita...
DAKTARI: Staki kujua hayo nataka kujua umevunjikaje mguu?
JAMAA: Dokta nisikilize kwanza, miaka kumi iliyopita nilikuwa nafanya kazi kwa bosi moja kule Uzunguni, siku moja binti yake mzuri sana akaja chumbani kwangu na kuniuliza kama nahitaji kitu chochote, nikamjibu sitaki, akarudia tena tena na kuniuliza tena kama sihitaji kitu chochote, mimi nikasema sihitaji kitu, akaondoka anacheka.
DAKTARI: Sasa hiyo inauhusiano gani na kuvunjika mguu?
 JAMAA:Sasa leo nilipokuwa niko juu ya mnazi nagema, si ndio jibu likanijia kwanini yule mrembo alikuwa ananiuliza lile swali, ndio bahati mbaya nikajisahau nikaanguka na kuvunjika mguu

DOGO NG'OMBE DUME YULE

Dogo kaenda likizo kijijini kwa babu yake. Siku hiyo babu kaamka asubuhi kamkuta dogo na glasi ya maziwa anainywa taratibu.
BABU: Umenunua wapi maziwa?
DOGO: Kwanini ninunue babu? Nimeenda kumkamua ng'ombe wako yule mweusi mimi mwenyewe
BABU: Lakini Dogo mbona yule ng'ombe ni dume?

DOKTA NILIKUWA NATAKA HIYO NYINGINE

Kamjamaa kasmati smati flani, kalienda hospitali kwa aibu aibu kakamuona dokta;
KAMJAMAA: Gud moning Dokta I am serious problem of health
DOKTA: Nini tena bwana mdogo?
KAMJAMAA: I want castration operation
DOKTA: Sikiliza, kwani hujui kiswahili? Hiyo operesheni sifanyi
KAMJAMAA: Dokta unajua mambo mengine ni siri so I talk English Please do me castration
DOKTA: Sitaki sioni sababu
KAMJAMAA: Dokta I pay you 1 milion shilings, mzee nisaidie
DOKTA: Dah haya japo kwa kweli sipendi kabisa...Jamaa wakati kalala dokta akamfanyia operesheni aliyotaka. Alipoamka dokta akampa maelezo
DOKTA: Sasa kama ulivyoagiza nimekufanyia castration  kama ulivyotaka, lakini nikagundua kuwa ulikuwa unatakiwa kuwa cirumcised pia kwa hiyo nimefanya hiyo pia
KAMJAMAA: Dokta nilikosea kusema nilikuwa nataka hiyo ya pili tu

MAUMIVU YAKIZIDIIIIIIIIIII............


1. Mkaka kaingia bar akakaa kaunta, wakati akiteremsha kitu roho inapenda, ghafla akaingia mdada ana sura mbaya sana kavaa kofia nzuri nyekundu;
MDADA: Mambo?
MKAKA: Poa, karibu
MDADA: Nikwambie kitu
MKAKA: Sema
MDADA: Ntakuuliza swali ukipata nakuwa mpenzi wako
MKAKA: Duh
MDADA: Nimevaa kofia rangi gani?
MKAKA: Nyeupe
MDADA: He jamani UMEPATAAAAAA


2. Baada ya kuona miezi inapita hapati haki yake kama mke mmama akaona ajaribu mbinu mpya;
MMAMA: mume wangu nakuuliza swali ukipata lazima ulale na mimi
MBABA: Uliza
MMAMA: kidoleni nimevaa nini?
MBABA: Tembo
MMAMA: Umekosea kidogo lakini sio kitu sana
Top of Form

16 October 2012

BREKINGNYUUUZ- WAMEIBA INJIN YA GARI LANGU

Tatizo ni kuwa nimezoea Volkswagen yangu injini iko nyuma sasa nashanga natafuta injini siioni sijui wamekwisha kwiba maana wabongo bwana hawana dogo wanaiba kila kitu. Watu ambao wanaiba vyuma vya daraja, mifuniko ya mashimo ya maji machafu, mabati ya vituo vya mabasi watashindwa kuiba injini? Lakini huyu mwizi ntampata tu

INDIKETA YAKO INAFANYA HAIFANYI

Jamaa alikuwa anapita Songea mjini,akapata wasiwasi indiketa ya nyuma haifanyi kazi, akasimamisha gari akamuomba mwananchi mmoja aangalie kama inafanya kazi;
MWANANCHI:Heb wash basi. Jamaa akawasha indiketa ya kushoto;
MWANANCHI: Hii indiketiinachekesha, inafanya kazi, haifanykazi, inafanya, haifanyi, inafanya, haifany
 

KISASI CHA UHAKIKA

Jamaa alikuwa anaumwa akapita kituo cha taxi akaikuta taxi moja, akamuomba sana taxi dreva ampeleke hospitaji lakini fedha yake ilikuwa ndogo, kitu cha ajabu dreva alimporomoshea jamaa matusi ya nguoni na kumwambia akapande bodaboda kama hana hela.
Wiki mbili baadae jamaa akawa amepona na anapesa mkononi, akaenda kituo cha taxi akakuta taxi nne ikiwemo ya yule dreva aliyewahi kumtukana, akamwendea dereva wa kwanza;
JAMAA: Natafuta dereva wa taxi shoga niondoke nae ntamlipa laki
DEREVA 1: We mwenda wazimu nini hebu toka hapa.. Jamaa akenda taxi ya pili
JAMAA: Natafuta dereva shoga niondoke nae ntamlipa laki
DEREVA 2: Pumbavu mkubwa toka hapa
Hatimae jamaa akaenda kwa yule taxi dreva aliyewahi kumtukana
JAMAA: Aise sijui unaweza kunipeleka Ubungo?
DEREVA: Ndio shilingi alfu kumi
JAMAA: Haya twende....wakati wanaondoka jamaa akahakikisha anapungia mkono wale madereva waliobaki kituoni huku akionyesha alama ya kidole gumba. Akiwaacha midomo wazi

TEMBO NA MPENZI WAKE SISIMIZI

Tembo na sisimizi walikutana kituo cha basi Mogomeni Mapipa wakapendana, wakaingia Luxury Bar na kuanza kunywa, baada ya mazungumzo ya hapa na pale wakakubaliana kuwa wapenzi na kuamua  kwenda kulala kwa sisimizi.
Bahati mbaya kuamka asubuhi tembo akawa kafia kwa mpenzi wake sisimizi. Jitihada za kuwapata ndugu zake zimeshindikana na serikali ya mtaa imemzilia sisimizi mwili. Huu ni mwezi wa tatu bado anachimba kaburi.

NADHANI MIE KUKU

MCHIZI: Mi nadhani mie ni kuku
DOKTA: Okay ni lini ulianza kudhani we kuku?
MCHIZI: Muda mrefu tu, toka nilipokuwa yai

NATAKA MAPACHA

Mmama alikuwa kapewa talaka na mumewe na akawa kadhulumiwa kila kitu, siku hiyo akawa pwani anapunga upepo kupunguza mawazo, zimwi likamtokea;
ZIMWI: Mbona una mawazo?
MMAMA: Sina kitu nimedhulumiwa vyote na mume wangu
ZIMWI: Nipe maombi matatu naweza kukupa chochote utakacho lakini mumeo wakati huohuo atapewa mara kumi zaidi.
MMAMA: Kwa uchungu sana, akasema naomba nyumba nzuri kando ya bahari yenye upepo mwanana.....na ikawa vile.
ZIMWI: Kumbuka mumeo kapewa mara kumi ya kwako
MMAMA:Haya nipe bilioni kumi...ikawa vile
ZIMWI: Mumeo kapewa mara kumi ya wewe
MMAMA: Ombi langu la mwisho naomba kuzaa mapacha

KUZIDISHA 35 NI MSALA

Kiukweli ni wazo zuri akina mama kuanza kuzaa wakiwa na miaka 20 na kuendelea, lakini utafiti umeonyesha kwa kweli ukifikisha 35 si vizuri kuendelea kuzaa. Matatizo mengi sana yataweza kukupata ukifikia kiasi hiki, kwanza ni nani anaweza kukubali kuwa baba wa watoto 35 na zaidi? Unaonaee, Je utaweza kuwalisha na kuwavisha na hata kuwalaza?. Kwa tangazo na ushauri huu ni makosa makubwa kuzaa zaidi ya watoto 35...JK umeonaee

TUNASAFISHA MASIKIO

Mambo ya Bongo, wako mpaka wasafisha masikiohela yako tu.

ITAKATIKA YENYEWE

Jamaa katika uhuni wake akakumbana na ugonjwa wa ajabu akavimba sehemu za siri, akaenda kwa daktari ambaye akamuangalia kwa makini;
DAKTARI: Umetembelea nchi ya Malawi karibuni?
JAMAA: Ndio dokta
DAKTARI: Na ukalala na mtu huko?
JAMAA: Ndio dokta
DAKTARI: Basi umepata ugonjwa unaitwa NYASALIASIS
JAMAA: Duh, dokta nisaidie nipone
DAKTARI: Ni ngumu kidogo maana wote waliougua ugonjwa huu wanakufa , lakini sijui labda tufanye operesheni.
JAMAA: Hakuna njia nyingine dokta, unajua hapo mahala pabaya, sasa kufanya operesheni hapo dah
DAKTARI: Jaribu sehemu nyingine lakini kwa kweli mi nadhani operesheni labda ingesaidia. Jamaa akatoka akaenda kwa mganga wa kienyeji
JAMAA: Aise nimepimwa nimekutwa na NYASALIASIS, sasa dokta anasema watanifanyia operesheni....Mganga akamwambia avue nguo, nae akamcheki, akaanza kucheka sana
JAMAA: Vipi mbona unanicheka?
MGANGA: Unajua madaktari wenu bwana hili tatizo dogo wanazunguka eti wanataka kukufanyia operesheni, yanini operesheni?
JAMAA: Utaweza kuniponesha?
MGANGA: Hapana, ila hakuna haja ya operesheni, mbona hii baada ya wiki itakatika yenyewe.

CHIMBA DAWA BUREEEE

Ndio kufanya nini?

UNA MIAKA MINGAPI?

MWANDISHI: Supasta una miaka mingapi?
SUPASTA: Nina miaka 20
MWANDISHI: He lakini si niliwahi kukuhoji miaka miwili mitatu iliyopita, na ukanambia una miaka 20?
SUPASTA:Si unaona mi sio muongo na nina msimamo bwana, nikikwambia kitu leo hata uje baada ya miaka mitano sibadili badili majibu kama wengine.

15 October 2012

WE NTOTO WEYEEE


Swaga za Mpemba anapofukuzia ntoto.’Ntoto weyeee Wallahi wanimalizaa,unrefuu kama nkarafuu, halafu wang’ara kama embe bolibo,nywelezo zinnyooka kama kamba za mibungo, kifua kintuna kama nazi koroma, miguuyo in jaa kama ndizi ya nkono wa tembo, he!  Nifikrie mwenzio naumiaaa miyeee

14 October 2012

MATANGAZO MENGINE BWANA

YAANI NI SWIM KWENYE MCHANGA? MNANITAFUTA UGOMVI? NAENDA KUSWIM KWENYE MAJI PAMBAF

BIA HOYEEEE

Kwanza naomba nitambue uwepo wenu wale watu wangu aka WABISHI DAMU unaonaee. Hawa watu wanaweza kununua ubishi, kubishana na redio, kubishana na magazeti, na kadhalika, kwa hiyo kabla ya kusema neno lazima utambue kwa heshima uwepo wao unaonaee. Uzuri wa watu hawa ni kuwa nchi yetu ina maendeleo makubwa kwa ajili yao, inalazimika sisi tusio wabishi kufanya kazi ya ziada ili japo kuwa wasiwe na ishu nyingi za kubisha unaonaee. Hawa watu wasingekuweko kama walimu wasingekuwa wanahamasisha wanafunzi kuwa na mijadala yenye mada kama zifuatazo;-
1. Baba na mama bora nani?
2. Jua na mvua bora nini? Unaonaee.  Mijadala kama hii ndio iliyoliingiza taifa letu katika janga la kuwa na wabishi hawa, ambao wengi siku hizi wanafanya shughuli za kugombania kushika nchi (....mmeshabisha dah...) unaonaee. Kwa kujua hilo ningependa kutangaza kuwa nimegundua kuwa vitu vingi hapa nchini vinaharibika kwa kutu, hebu fikiria mpaka vituo vya mabasi vinaanguka kwa kuliwa na kutu,madaraja, nondo, mageti, magari , vyote vinaharibiwa na kutu, na hata wabishi mtakubali maji ndio yanayoleta uharibifu huu mkubwa. Kwa kweli jibu ni wazi kabisa MAJI NI KITU CHA HATARI. Uliwahi kusikia bia imesababisha kutu? Au ukasikia oh kile kibanda cha kusubiria mabasi kimeanguka kwa kumwagikiwa na bia? Natangaza rasmi kampeni ya ACHANA NA MAJI KUNYWA BIA , MAJI YANALETA KUTU. Unaonaee  HAYA ANZENI KUBISHA KAMA KAWAIDA YENU

13 October 2012

BREAKING NEWSSSSS WAFANYAKAZI WAGOMBANIA BLOG

Hii blog www.chekanakitime.blogspot.com itaniletea matatizo makubwa unaonaee. Nimepigiwa simu na bosi mmoja toka nchi jirani kuwa ninapunguza muda wa watu kufanya kazi katika kampuni yake kwa kuwa wafanyakazi wake imekuwa kama ni lazima kila asubuhi waanze siku kwa kuangalia nini kipya kimo kwenye blog. Kwa maelezo ya bosi mwenyewe Bwana Aziz, juzi kulitokea ngumi ofisini kwani muhudumu wa chai aliwahi kuwasha compyuta ya sekretari akawa anawahi kusoma habari mpya na ukatokea ugomvi wa kurushiana vikombe vya chai kati yake na sekretari ambaye alihoji mama chai kapata wapi pasiwed yake, ambayo ni mwaka wa kuzaliwa wa mume wake, ugomvi huu ulishika kasi baada ya ofisa usafi kuja na mop bichi na kumzaba nalo meneja utumishi ambaye alionekana akisisitiza watu wasiwe wanaangalia blog zozote nchini. Kwa kweli baada ya hapa ofisi ilichafuka kwa kila mtu kutafuta upande wa kusaidia ingawaje inaonekana sababu zilibadilika kidogo maana, yule binti wa masjala alisikika akisema ,'Ukome kuchukua mabwana wa watu, cha ajabu alikuwa anampiga na mafaili kijana ambaye aliingia tu kwenye ofisi hiyo kwa shida ambayo haijaeleweka mpaka tunakwenda mitamboni. Kwa kweli ni busara za mzee mlinzi tu ndio zilizozima vurugu ile. Kama bosi wa blog ntakaa na washauri wangu kuona tuongeze kipengele kipi ili kuweza kuamsha hisia kama hizi katika ofisi nyingine. Wasalaam

UKIJARIBU MI SIMO OHOO


ANZA TU KUZOEA MAKABURI

Baada ya kuona afya yake inatetereka, mlevi mmoja akenda hospitali kupimwa;
DOKTA: Mheshimiwa tumekufanyia vipimo vyote na nasikitika maini yako na figo zote zimeshaharibika kabisa hivyo tunadhani huwezi kuishi zaidi ya siku kumi
MLEVI: Dah dokta, hata nikiacha pombe? Au niwe nakunywa maziwa tu? Kwani hakuna dawa yoyote au msaada wowote?
DOKTA: Labda pengine uanze kushinda makaburini
MLEVI: Dokta hiyo itasaidia?
DOKTA: Hapana haitasaidia, lakini japo itakusaidia kuanza kuzoeazoea mazingira

MLEVI KAOKOTA FUVU

Mlevi kapita karibu na makaburi akaokota vufu la kichwa, haraka akapiga simu polisi.
MLEVI: Afande, njooni haraka nimeokota fuvu la binadamu hapa makaburini
POLISI: Haya tunakuja itakuwa kuna mtu kafukua kaburi
MLEVI: Ndiyo, halafu nimechunguza kwa makini, inaonekana marehemu alikuwa na pembe ndefu kama za ng'ombe

SIJUI WAMENILOGA???

Jamaa kaingia bar moja kwa moja kakaa kaunta. Akaagiza chupa nne za safari. Akazimaliza chapchap, akaagiza chupa tatu, akazimaliza. Akaagiza chupa mbili akamaliza akaagiza chupa moja akawa anaiangalia sna kwa makini wakati huo akiwa kisha lewa sana.
MUHUDUMU: Vipi imekushinda
MLEVI: Mi nashangaa sana,nikiwa na bia nyingi naweza kunywa, nikiagiza bia chache nashindwa kunywa halafu nalewa, sijui wameniloga

MR IBU VIPI TENAAAAA?


12 October 2012

WAZAZI WANANILAZIMISHA NIMUOE RIHANNA

Nina mpango wa kutafuta njia ya kufunga inbox ya Facebook yangu,ni kweli kuna watu wengi wanaomba ushauri kwangu na najitahidi kutoa majibu, lakini wengine maswali yao magumu hebu tumsome huyu jamani sijui nimwambie nini---Anko J nina tatizo, Beyonce kanipigia simu kunitaarifu kuwa ana mimba yangu, nimewaambia wazazi wangu wamekataa kata kata nisimuoe eti keshakuwa sekand hend, na kama nataka basi nimuoe Rihanna , lakini mie Rihanna simtaki maana toka nimeanza kutoka nae nilisha pata fununu kuwa ananisaliti kwa Chris Brown, Anko nifanyeje? sitaki kuwaudhi wazazi wangu

11 October 2012

JE, BIA INA FAIDA?????????

Tafakari chukua hatua. Hakuna ubishi kama kuna giza ni wazi kutakuwa na mwanga. Kama kuna wafupi ni wazi kuna warefu, na hivyo basi kama kuna warembo ni wazi kuna *******umeonaee. Sasa bia ni kitu kizuri sana kwa kuwa hawa warembo huwa hawana tabu kupata wenza, ila hawa********.wanapata tabu sana kupata wenza. Bia ni msaada mkubwa sana. Mtu ukisha kunywa bia za kutosha hawa********wanageuka warembo, na kwa hiyo wanapata haki sawa kama warembo. Kwa mantiki hiyo bia ni kitu muhimu sana QED

HURUMA YANGU NI MUHIMU KWA MAISHA YAO

Kuwa na huruma sana inaponza sana, kwa mfano wa karibu ni mimi. Unajua mimi ni mtu mwenye huruma sana, na hii inanikosti. Lakini bahati mbaya hiyo ndio tabia yangu, siwezi kubadilika. Unajua kwa mfano isingekuwa huruma yangu ya hali ya juu leo hii ningekuwa sinywi pombe kabisaaaa unaonaee. Lakini mara nyingi nikiwa na glasi ya mwisho ambayo huwa najisemea baada ya glasi hii sinywi tena, utaona huruma yangu inaanza kunisuta. Maana naanza kufikiria ni watu wangapi ambao maisha yao yanategemea wanywaji kama mimi kuendelea kunywa? Kuna wakulima wa ngano ambao ikiwa wanywaji wote tutaacha kunywa na wao watakosa kipato cha kuuza mazao yao kwa watengeneza pombe, maisha ya watoto wao itakuwaje? Haya baada ya hapo kuna hizi kampuni za kutengeneza pombe, tena siku hizi ukienda kwenye makampuni makubwa kuna wakurugenzi, wakurugenzi wasaidizi, kaimu wakurugenzi, mameneja, wahasibu , wahudumu wa ofisi, madreva, wafanyakazi viwandani, watu wa masoko, wenye baa, wahudumu wa baa, yaani nikiwaza kuacha pombe naanza kufikiria watoto wa hawa watu wote wananitegemea mimi, halafu kitendo cha kufanya ukatili mkubwa wa kuwanyima haki yao ya kuishi kwa ajili ya ubinafsi wangu tu kinanisuta sana? Tena siku hizi unakuta mpaka wasanii toka nje wanatakiwa kuja kuponea fedha zangu ili watoto wao waende shule, kwa kweli huruma yangu naona ni muhimu kuliko ubinafsi wangu. na hapo ndipo huwa naagiza nne mfululizo, sio kwa sababu napenda pombe jamani ni huruma kwa hawa wote ambao maisha yao hapa mjini yananitegemea umeonaee. Tujitahidi jamani ili kusaidia wenzetu

10 October 2012

BAADA YA NYANI KUVUTA BANGI..........

Siku moja Nyani alikuwa kakaa kijiweni anavuta bangi. Mjusi akaja akampa 'Hi', akaomjoin na kuomba puff, nyani akamuonya kuwa ile bangi kali ni kipisi cha kutoka Makete. Mjusi akapokea wakaanza kuvuta kwa raha zao. Mjusi akawa hoi kwa stimu akamwambia nyani,'Nasikia koo limekauka ngoja niende mtoni nikanywe maji'. Mjusi kufika mtoni kwa kuwa alikuwa na stimu nyingi akatumbukia mtoni. 
Mamba aliyekuwa pembeni akamwona akawahi kumuokoa na kumtoa nje ya maji. Mamba akamuuliza mjusi imekuwaje kutumbukia mtoni kizembe vile, mjusi akajibu, 'Nilikuwa na nyani tunavuta bangi nikasikia kiu cha ajabu nikajikuta kwenye maji' mamba akasema, 'Hebu twende kwa huyo nyani'. Wakamkuta nyani ndo anamalizia kile kipisi hata macho tabu kufungua. Mamba akamuita, 'Oya'. nyani akafungua macho alipomuona mamba akashtuka sana,'Mshikaji umekunywa maji debe ngapi umerudi mkubwa hivyo?


ZILE MVUA ZILIZOTANGAZWA JANA ZIMETUKOSAKOSA


NI WAKTI WAAAAA KUCHEKA-HUKU-UNALIA (1)

Mkuu moja, wale wa karibu na juu kabisa, alikuwa na uhusiano wa kikomedy komedy na sekstari wake unaonaee, kiasi cha kwamba mdada akawa mwisho wa mwezi anenda wa keshia na kuchukua mshahara wa Mkuu kwa niaba yake teh teh teh, sasa basi si siku hiyo Mkuu akawa kule kwenye mji wenye mnada wa nyama siku za wikiendi, mkewe akaugua, mzee akamwambia kachuk
ue mshahara wangu kwa keshiii...keshia unaona, kumbe by then wakati huo si yule sekstari ameshachukua ile salari ya mzee yote. Sasa mke alipofika kwa keshia kuomba mshahara, keshia macho yakamtoka kama mjusi aliyebanwa na mlango , even then akatumia akili ya ziada akarash kwanza kwa seksetari, kumuuliza kuhusu ule mshahara, seksetari akajibu tena kwa nyodo, mpigieni bosi wenu mwambie mie nilishachukua huo mshahara habari ndio hiyo, keshia akarash kwa thief akauntant, sori chief akauntant, akampa ishu nzima, dah thief eh chief akauntant akamwambia keshia toa hiyo hela popote maza asishtuke aondoke, hayo mengine tutasov. Mama akaondoka. Alipoondoka maza kikao cha ofisi kikafanyika chapchap, sekstari akapigwa transfa ya juu juu kwenda ofisi nyingineeee, chini ya bosi mwingineee, na akaambiwa nakatwa ule mshahara aliochukua kwa niaba ya mubosi unaonaeeeee

BAADA YA KITAMBAA CHEUPE SASA NI CHUPI NYEUPE

Kitambaa cheupe ni kitambaa ambacho hung'aa vizuri sana na wanamuziki wamekuwa wakikitumia kama uniform, kama wanavyoonekana Wananjenje katika picha hii, na King Kiki alikipandisha shati kwa wimbo wake maarufu Kitambaa cheupe, ambapo alikuwa akiwahamasisha wapenzi wa muziki kutembea na kitambaa cheupe na kukiinua na kukionyesha wakati akiimba wimbo wake huo maarufu. Karibuni kumekuweko na maendeleo mapya ya kitambaa cheupe ambapo wanamuziki wabunifu wametumia kitambaa hicho kushona chupi ambazo nao kwa kutumia mtindo wa Mzee Kiki wameanza kuonyesha wapenzi wa muziki wao. Blog hii maarufu kwa kucheka mpaka machozi yatoke inasubiri wanamuziki hawa kama nao watawahamasisha wapenzi wao wa muziki kuvaa chupi nyeupe na kuzionyesha wakati wanacheza kwa huu mtindo wao mpya ambao magazeti ya nanili yanadai unaitwa 'UNAKULAGA?" Mdau mmoja wa muziki alisikika akisema lazima nae ashone chupi nyeupe ili akaionyeshe kwenye show ijayo....je na sisi Tanzania tumegundua staili mpya itakayotingisha katika ulimwengu wa muziki duniani? Je chanel O watatupaisha au watatubania? Je Wanaijeria wataachana na Azonto wajitose kwenye huu mtindo mpya wa 'UNAKULAGA'?

MWANAUME UNAPOPATA KIBANO TOKA KWA MAMA

Kwa kawaida wanaume hudhani kuwa wakianzisha ngumi na akina mama lazima washinde. Lakini hadithi hii si kweli. Ushauri kwa wanaume usilianzishe na akina mama mambo yanaweza kukugeukia ukashangaa unapewa kibano cha mbwa mwizi. Na hasara ya ziada ya kipigo hiki ni kuwa baada ya hapo kila mtu anaendelea kukucheka. CHONDE WABABA KUPIGANA NA WAMAMA HAILIPI.
Mbaya zaidi ni pale mwananume ukiwa mlevi tu huna faida yoyote, wenyewe wanaita MWANAUME SURUALI, hapo utakuta jitu halijaacha chochote nyumbani lakini likirudi limelewa linadai chakula na kulalamika eti,'Mbona nyama hazitoshi? Ugali mdogo' na kadhalika.. kiukweli unaweza kupata kibano cha kueleweka ukakumbuka enzi ulipokuwa shule ya msingi. halafu wamam wana katabia ka kukimbilia kushika ikulu, hii humaliza nguvu kabisaa, tena unaweza mwanaume mzima ukaachia kojo la nguvu kwa maumivu....all in all usianzishe ngumi ohooooo

9 October 2012

KWA WAVAA VIMINI TU

NDUGU WAPENZI WA VIMINI, SIDHANI KAMA MNAWAZO KUWA IKO SIKU MTAZEEKA, KWA TAARIFA YENU KUZEEKA LAZIMA HATA KAMA UTACHEZA JUKWAANI BILA NGUO, MNAONAEEE. SASA BASI NAWATAARIFU MKUMBUKE UZEE UNAKUJA NA SURA KUKONGOROKA MNAONAEE, LAKINI VIMINI VITAKUWEKO KWA HIYO NINATABIRI KUWA MTAKUWA KAMA BIBI HAPO JUU, BISHENI KAMA KAWAIDA YENU

NICHAGUENI MIMI

MGOMBEA: Ndugu wananchi nichagueni muone, maana nchi hii viongozi wamekuwa mafisadi, wala rushwa, wanajaza matumbo yao tu, wanajitajirisha bila kujali sisi wananchi wa kawaida
MWANANCHI: Kwa hiyo tukikuchagua utayaondoa yote hayo mara moja?
MGOMBEA: Unajua mambo haya magumu, yanataka kwanza ujiunge nao ili ujue siri na mbinu zao ndipo hapo utakapojua namna ya kuyaondoa

SWAGA ZA POLISI ANAPOMSOMESHA DEMU


Unajua nakuthamini zaidi ya rushwa na posho, bira ya wewe mimi siwezi kuishi, ni sawa na kukosa bunduki eneo ra tukio,nakuheshimu kama ninavyoheshimu rindo, wewe ndio IGP wa moyo wangu. Mbona upo kimya, nina RB ya penzi rako, nijibu nifungue jarada rako ndani ya moyo wangu. Usifanye moyo wangu ukaenda mbio kama difenda mpya,. Nakuhakikishia ntakuwekea usarama kama msafara wa Rais, usiniweke roho juu kama maandamano ya CHADEMA nijibu poti.