PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

FISADI MTAKATIFU

Kuna ndugu wawili ambao kiukweli walikuwa mafisadi wa hali ya juu, lakini walitumia utajiri wao huo kuficha ubaya wao, na wakawa wahudhuriaji wazuri wa kanisa ili waonekane ni watu wema. Bahati mbaya mchungaji wao ambaye alikuwa akiliongoza kanisa lile kwa muda mrefu akafariki akaja mchungaji mpya ambaye pamoja na kuwagundua mapema kuwa wale ndugu ni wanafiki, akaanza kuliendesha kanisa vizuri kiasi cha watu kuanza kuongezeka, hivyo ikalazimika kuanzisha harambee ya mchango kwa ajili ya kupanua kanisa. Mmoja wa wale ndugu akafariki wakati ule, mwenzake akamuendea mchungaji;
FISADI: Mchungaji, hapa nina cheki ambayo italipa gharama zote za ujenzi wa kanisa, lakini siku ya kumzika ndugu yangu italazimu umtangaze kuwa alikuwa ni mtu MTAKATIFU.........Mchungaji akapokea cheki kwa shukrani nyingi na haraka sana kuipeleka benki. Siku ya mazishi taratibu zote zikafuatwa hatimae mchungaji akaanza kutoa mahubiri
MCHUNGAJI:Hakuna siri kuwa marehemu alikuwa anaendesha genge la majambazi, alikuwa mwizi wa mali za umma , dhulumati, alikuwa muasherati mkubwa,mshirikina, ameharibu mabinti wetu wengi kwa fedha zake, alitumia rushwa kwa kufanikisha mambo yake, wote tunajua hakuwa mwaminifu kwa ndoa yake na mengine mengi. Lakini niwe mkweli, huyu bwana alikuwa MTAKATIFU ukilinganisha nandugu yake ambaye bado yuko hai.

Comments