HATUPIMI BANDO

30 September 2012

UNA BAHATI SANA -2

Mdada alikuwa akisafiri kwenye basi, ghafla Jamaa aliyekuwa kakaa kiti cha nyuma akamtapikia
JAMAA: Samahani dada lakini una bahati sana
MDADA: Mshenzi mkubwa umenitapikia halafu unasema nina bahati
JAMAA: Ndio leo nimetoka kula pilau, kwa kawaida saa hizi huwa nakuwa nimekunywa kangara

UNA BAHATI SANA 1

 Jamaa kagongwa na baiskeli, mwendesha baiskeli akaanza kumnyanyua jamaa;
MWENDESHA BAISKELI: Aise una bahati sana
JAMAA: Umenigonga na baiskeli halafu unanambia nina bahati
MWENDESHA BAISKELI: Ni kweli maana kwa kawaida huwa naendesha daladala
 

DEREVA WA BODABODA KAVUNJIKA SHINGO

Mwendesha Bodaboda aliamua kugeuza koti lake liangalie nyuma ili kukinga upepo, bahati mbaya akapata ajali mbaya ya kugonga mti, TRAFIKI akaja akawakuta watu wawili ambao walisema kuwa walikuwa wa kwanza kufika eneo la ajali;
TRAFIKI: Kwa hiyo mlimkuta katika hali gani huyu kijana?
MWANANCHI: Kwa kweli tulimkuta akitapatapa akilia kwa maumivu. Kitu tulichogundua mara moja ni kuwa shingo yake iligeukia mgongoni, tukajitahidi kuizungusha mpaka ikarudi mahala pake, lakini maskini akakata roho

MARUFUKU KUPATA MIMBA

Mashosti wawili wanazungumza;
SHOSTI 1:Yaani mwenzio nina mtihani kweli wa kujitahidi nisifanye kosa nikapata  mimba
SHOSTI 2: Ai shostiii si ulinambia mumeo hana kizazi
SHOSTI 1: Tatizo ndio linaanzia hapo, nikipata mimba tu kimenuka

29 September 2012

SIDIRIA UNAVAA YA NINI?

MKE: Mume wangu ninunulie sidiria
MUME: Acha vichekesho, tuwe wakweli unataka kuvaa sidiria matiti yenyewe yako wapi?
MKE: Usinitafute niseme, wewe kaptura unavaa ya nini? au unanitafuta niseme
MUME: Basi mke wangu nilikuwa nakutania tu

27 September 2012

JONGOO KAKATAA KUPANDA MTUNGI

Jamaa alioa kwa furaha nyingi na vifijo na hatimae kuanza kuendelea na maisha yake. Lakini hata wiki mbili hazikupita ndoa ikaanza kuwa chungu maana kila alipokuwa nyumbani mke alikuwa anataka. Asubuhi, mchana, jioni mke alikuwa anadai haki yake, jamaa alikuwa kachoka kabisa kabisa, hata kazini akawa hana raha. Na mke akamwambia kuwa anataka mtoto na mchakamchaka utaendelea mpaka mtoto apatikane. Hatimae jamaa alifikia wakati hata jongoo akaacha kupanda mtungi, nyumbani pakawa hapakaliki. Akamwambia rafiki yake aliyempeleka kwa mganga mmoja;
MGANGA: Hili tatizo lako nilikuwa na dawa yake lakini imeisha imebaki kidogo itakayotosha jongoo kusimama mara tatu tu.
JAMAA: Hata hiyo itatosha mzee nyumbani kumekuwa jehanamu.
MGANGA:(Akatoa unga fulani) Huu paka sasa hivi kwenye jongoo, baada ya hapo  ukitaka kutumia jongoo sema tu BRAAAAAAM atasimama, ukitaka atulie sema BRAAAAM BRAAAAAAM......jamaa akapaka ule unga akaona ajaribu
JAMAA: BRAAAAAAAM loh hatari kubwa kidogo vifungo vya lisani vifunguke, jamaa akafurahi sana. BRAAAAAM BRAAAAM jongoo akatulia, akaingia kwenye gari lake kuwahi home, akajua ana mara mbili zimebaki. Akasimama kwenye traffic lights, si ikaja pikipiki ikapiga BRAAAAAAAAM, jongoo kainuka, jamaa kachanganyikiwa, kabla hajafanya lolote pikipiki ikalia BRAAAAM BRAAAAM ikaondoka na jongoo akatulia. Jamaa akawahi home akijua imebakia nafasi moja tu. Akaingia kwake akaoga vizuri akamuita mkewe;
JAMAA: Mke wangu njoo, (mke alipoingia tu), BRAAAAAAAM
MKE: Hakuna cha BRAAAAAM BRAAAAM nataka haki yangu...........jamaa akaanza kulia

NYAU KAKOJOLEA CHAKULA CHAKO

Mbaba mmoja alikuwa mezani anakula na binti yake wa miaka mitano, simu ikalia, akanyanyuka kwenda kusikiliza pembeni, aliporudi binti yake akaanza;
BINTI:Baba nikwambie kitu?
BABA: Nyamaza nimekukataza mara ngapi kuongea wakati unakula? Maliza kula kwanza halafu utaniambia....wakaendelea kula walipomaliza;
BABA: Haya ulikuwa unataka kuniambia nini mwanangu?
BINTI: Wakati umeenda kuongea na simuuu, nyau alikojolea chakula chako

UKINIPIGA UTAONA

Kipofu kampiga mtu mpaka kamuua, akafikishwa mahakamani;
HAKIMU: Kwanini umefanya ukatili namna hii
KIPOFU: Mheshimiwa marehemu alisema mwenyewe,'Ukinipiga utaona', kwa vile nilikuwa na hamu kubwa ya kuweza kuona, nikajitahidi kumpiga sana  ILI nipone, bahati mbaya kafariki.

ONDOKA HARAKA MUME WANGU ATARUDI WAKATI WOWOTE

Jamaa akiwa nyumba ndogo karelax na Mdada, Mdada kwa sauti laini akaanza;
MDADA: Jamani lini utanyoa hizo ndevu, mi sizipendi
JAMAA: Bwana ziache mke wangu anazipenda sana hatutaelewana nikizinyoa
MDADA: Nyoa jamani, au hunipendi?
JAMAA: Nakupenda, lakini kwanini huzipendi?
MDADA: Unajua we hendsome some sana mpenzi, mi nataka niwe nauona uso wako wote swiry...hatimae jamaa akanyoa ndevu zote. Baadae akarudi nyumbani usiku akanyata taratibu na hatimae akapanda kitandani akalala. Mke wake akiwa usingizini akageuka na kumgusa mashavu
MKE: We James, huogopi kufa, mume wangu atarudi muda wowote, ondoka haraka bwana

KAMUSI YA MAPENZI YA KIBONGO MOVIE

LOVE DICTIONARY YA KIBONGO MOVIE
Honey-Kimeo
Dear-Wakuzugia
Sweety-Mshamba
My Fiancee- Zezeta
Baby- Jinga
Darling- Bwege
Husband- Buzi
Chunga sana jina lako

HAWEZI KUNIOA SI 'TYPE' YANGU

Dear Mzee Cheka Na Kitime,
Nategemea barua hii itakukuta salama. Mimi ni msichana wa miaka 23. Nilifiwa na wazazi wangu wakati nikiwa na miaka minane. Bibi yangu alishindwa kunilipia shule hivyo nikawa nyumbani tu, bahati nzuri mvulana mmoja kijijini kwetu akanambia atanisaidia, wakati huo alikuwa anauza machungwa barabarani. Kweli alianza kunilipia shule, miaka yote, hatimae hata yeye akabadili kazi akaanza kuendesha daladala, na ameendelea kunilipia mpaka sasa niko chuo kikuu. Namshukuru Mungu kwa kunikutanisha na malaika kama huyu sijui siku hizi ningekuwa wapi
Tatizo langu ni kuwa anataka kunioa nikimaliza chuo, na mimi kwa kweli nashindwa kumwambia kuwa itakuwa vigumu kwa kuwa yeye siyo 'type' yangu. Hebu fikiria mimi ni graduate halafu naolewa na dreva wa daladala, ni wazi kuwa si type yangu. Ninachoomba ni busara zako ntamwambiaje bila kumuumiza, kuwa haiwezekanai mimi nikaolewa na yeye?

HUYU MKE WANGU WAKO BADO SUBIRI

Jamaa alikuwa kwenye taxi akapita nje ya bar moja yenye guesthouse akamuona mkewe akipotelea ndani ya hiyo bar;
JAMAA: Dreva simama. Unataka laki tatu ya chapchap?
DREVA: Bila shaka mzee
JAMAA: Mke wangu kaingia kwenye ile bar, picha yake hii, ingia mtoe tena kwa umlete hapa ukiwa unamtandika vibao.......dreva akatoka na baada ya dakika chache akatoka anamburula mwanamke na makonde juu,
JAMAA: Mbona umekosea huyo siyo mke wangu umeshaharibu mambo
DREVA: Najua, huyu ni mke wangu, sasa ndio naenda kumtoa mkeo

25 September 2012

NI VIZURI WATOTO WAANZE MICHEZO WAKATI WADOGOHAHAHAHAHA HUYU NI MIMI

Walevi wawili walikuwa wanayumba barabarani, mmoja akaokota kioo, akaangaliaa;
MLEVI: Hii sura kama naifahamu, ila jina limenitoka kabisaaaa
MLEVI 2 akachukua kile kioo akaangalia akacheka sana;
MLEVI 2: Hahahahahaha yaani ukisikia mlevi ndio wewe, huyu ni mimi hapa, yaani umelewa mpaka hata mimi umenisahahu hahahahahah

BLUES LA GRADUATION YA FORM FOUR

Ilikuwa siku ya mahafali ya kidato cha nne, mambo yalikuwa mengi na hatimae jioni ikafika disco likafunguliwa rasmi. Muziki taratibu wa blues ukawa unalia, MIDIMAN akasimama na kumnyanyua mdada mmoja ambaye alikuwa  anachukua mchepuo wa sayansi, katikati ya blues umeme ukakatika;
MIDIMAN: What is the matter?
MDADA: Matter is anything which has weight and occupy space

UTALIPA HULIPI? 1


DOKTA NAUMWAAAAA

BABU:Dokta nina tatizo la kujambajamba, lakini bahati nzuri, nikijamba hakuna harufu wala sauti, na huwezi kuamini toka nimeingia humu kwako nimeshajamba mara tatu
DOKTA akaandika kwenye karatasi...
DOKTA: Tafuta dawa hizi kisha rudi baada ya wiki 2
BABU: Ntaakuwa nimeacha kujamba?
DOKTA: Hapana ila pua zako zitakuwa zimepona utaanza kusikia harufu, kisha baada ya hapo ntakupa dawa ya masikio uwe unasikia vizuri zaidi

PRESS MAANA YAKE SI BONYEZA?

Mwandishi wa habari mdada, juzi juzi akiwa na kamera yake katikati ya kundi la wananchi, alikuwa akiwahoji maswala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Mdada huyu kifuani alikuwa kavaa nembo imeandikwa PRESS. Mwananchi mmoja ambaye alikuwa amekwisha onja pombe kwa sana, akaminya tena na tena pale palipoandikwa PRESS, hata polisi walipomkamata alisisitiza kuwa PRESS tafsiri yake ni BONYEZA, hivyo anawashangaa hawa askari kumsumbua anapotimiza wajibu wake kama mwananchi.

24 September 2012

BREAKING NEWS-Una habari kuwa una ndugu yako Mchina?

Wataalamu wa uwingi wa watu duniani wanasema katika kila watu watano duniani mmoja ni Mchina. Je, familia yako ina watu wangapi? Kama mko watano ujue ndugu yako mmoja ni Mchina, hebu jaribu kuwakumbuka ndugu zako nani unaemuona wa Kichinachina?

ZUZU NA BABA ZUZU

ZUZU: Baba leo nimekuwa mjanja, sikupanda daladala, nikawa nalifukuza tu mpaka nimefika hapa kwa hiyo mfukoni nina shilingi mia hamsini
BABA ZUZU: Pambafu ungekuwa na akili ungefukuza taxi saa hizi ungekuwa na shilingi alfu kumi

23 September 2012

MLEVI KATUMBUKIA KWENYE KABURI

Mlevi alipita makaburini usiku akaangukia kwenye kaburi lililokuwa limetayarishwa kuzikia kesho yake...akajitahidi kutoka akashindwa, akaamua alale kesho yake atapata msaada. Nusu saa baadae mlevi mwingine akatumbukia mulemule, akawa anajitahidi kutoka lakini akawa anatereza, mlevi wa kwanza akaamka akamkuta mwenzie anahangaika kutoka;
MLEVI 1: Afadhali upumzike tu, mi mwenyewe nimejitahidi kutoka nimeshindwa.....mlevi wa pili kusikia hilo alipata nguvu za ajabu na kutoka kwa mbio za ajabu

SORI MKE WANGU POMBE MBAYA

WIFE alikuwa kaingiza mwanaume kwenye chumba chake cha ndoa. Wakiwa wamelala mume akapiga hodi, jamaa akapanik;
WIFE: Tulia huyu ni mlevi kiasi akiingia humu hataweza kukuona... mume akaingia akiwa njwii, akavua nguo zake na kuingia kitandani bila kulalamika, ghafla akshtuka alipoangalia miguuni
MUME: We mbona kuna miguu sita? Kuna nini kinaendelea?
WIFE: Ulevi wako huo sasa umezidi, mi naona miguu minne hebu amka toka kwenye kitanda uhesabu vizuri.....MUME akaamka na akaanza kuhesabu;
MUME: Moja , mbili , tatu, nne aaah kweli, sori mke wangu hizi pombe zinanipeleka pabaya

TUANZE KWA KUKOPI END PEST


22 September 2012

DOKTA NAUMWA

MGONJWA: Dokta nikinyanyua mkono kidogo unauma sana.
DOKTA ALIYEKO KWENYE MGOMO:Basi usiunyayue

KANITAPIKIA AKANILIPA

Mlevi kamkuta mlevi mwenzie analia nje ya baa;
KOLU: We vipi tena unalewa mpaka unalia? Au umeishiwa hela ya kunywa nikakununulie?
DOLU: Nimejitapikia, mke wangu mkorofi nikifika atanidunda sana.
KOLU: Tumia akili, chukua noti ya alfu kumi, weka kwenye mfuko wa shati, ukifika hom mwambie mkeo kuna mlevi alikutapikia akakulipa alfu kumi kaweka kwenye mfuko wa shati akiiona atakuelewa.....DOLU akakubali kisha akaelekea kwake, alipofika mkewe kumuona tu;
MKE: We mshenzi, leo umelewa mpaka umejitapikia, utanitambua.
DOLU: Subiri mke wangu kuna mlevi alinitapikia akaniomba msamaha akanilipa alfu kumi iko kwenye mfuko wa shati....MKE akaingiza mkono kwenye mfuko akakuta shilingi alfu ishirini.
MKE: We si umesema alikulipa alfu kumi mbona kuna alfu ishirini?
DOLU: Unajua kwa bahati mbaya aliniharishia pia kwa hiyo akaongeza hela

SIJUI NIFE?

Text messages za leo;
MDADA: Baby naomba credit ya elfu tano nataka kumpigia simu baba Arusha.
MDADA:Baby nakuja geto niandalie chips na kuku mzima nakuja na friends wangu, alafu nadaiwa elfu 35 nilikopa mpenzi wangu, mwenyewe ntakuja nae achukue.
MDADA:Baby please naomba elfu25 ya saluni si unajua leo weekend, I love you mwaahhhhhhhh.

21 September 2012

MTANI TOKA JIRANI ANAMPA SIFA BINTI

Ntoto veyeee wallahi wanimalizaaa, unrefu kama nkarafuu, halafu wang'ara kama embe boribo, nywelezo zinnyooka kama kamba za mibungo, kifua kintuna kama nazi koromaaaa. Miguu in jaa kama ndizi ya nkono wa tembo heee, nifikirieeee mwenziooo naumiya miyeee. Tukutane Forodhani magharibi nkununulie urojooo

MKE WANGU HAJAJUA

RAFIKI: E bwana mbona unaonekana huna raha?
JAMAA: Karibuni nitaanza kuitwa baba
RAFIKI: Hilo jambo la heri na unatakiwa uwe na furaha, mkeo anasemaje?
JAMAA: Mke wangu hajui hii habari bado

WIFE ALIPATA TEXT YAKO?

JAMAA:Mi namuacha mke wangu
RAFIKI: Kwanini?
JAMAA: Mi nilisafiri, wakati narudi nikamtumia text, na kumtaarifu ntarudi saa ngapi, cha ajabu si nimemfumania na bwana tena chumbani kwetu
RAFIKI: Usichukue uamuzi wa haraka, je una uhakika alipata text yako?

20 September 2012

BABY,SWIRY UNAJUA LEO BIRTHDAY YANGU

Jamani huu wizi 'live', nimekaa nae muda mrefu tumekunywa sana, sasa nataka kulipa bili, nimetoa bulungutu la noti nachagua zile zilizochoka choka ndio nilipie, naona mkono uko shingoni, na kwa sauti ya kumtoa nyoka shimoni;
MDADA: Swiry, darling baby unajua leo kumbe birthday yangu

BABY NAMBA YAKO NGAPI?


Huyu mpenzi sasa nimeamua tuachane maana kama ujinga hapa ndio makao makuu, siku moja, aliniiuliza ‘ Hivi naweza kumuua samaki kwa kumzamisha kwenye maji?’ sikumjibu maana niliona heri ninyamaze, jibu langu linaweza kuonekana tusi. Leo kanipigia simu mapema asubuhi, eti ananiuliza,'Samahani Baby namba yako ya simu ngapi? Nikumbushe mie nimeisahau'

MAMA KAKOSA NINI?

Mtoto kaingia chumbani ghafla kakuta wazazi wake wako bizi.
MTOTO: Mnafanya nini?
BABA: Nampiga mama
MTOTO: Hee, Mama asubuhi kapigwa na anko Deo, halafu akapigwa na polisi, halafu tena akapigwa na babu wa mkaa kakosa nini leo?
BABA kabaki mdomo wazi, mkewe kazimia

19 September 2012

COMING SOON

Yanki kamuomba baba yake fedha za matumizi;
YANKI: Oyaa dingi, fanya mambo mi nipe mkwanja naenda kutana na washkaji kujiachia
BABA: Pumbavu mkubwa na kwa lugha yako hiyo sikupi hata senti tano mpaka nife
YANKI: Poa dingi mi na weit ufe. Niko one man alone sitishiki.......yule yanki akenda kuchukua picha ya baba yake na kwenda nayo mpaka makaburini, akatafuta mti mmoja mkubwa katikati ya makaburi kisha akapigilia picha ya baba yake kwenye mti huo na chini akaandika ' COMING SOON"

USHAURI KWA WENYE KIGUGUMIZI

Ikiwa una kigugumizi ni vizuri ukajifunza kukwepa maneno ambayo yatakuletea matatizo, kwa mfano itanaweza kukukosti ukiingia katika mgahawa ukaamua kuomba juisi ya matango, pia ukikuta mdada anauza matikiti, we pita tu usianze kusifu ukubwa wa matikiti hayo, ni kitu cha hatari. Ukiwa una shida ya visa ya kwenda Uchina, wewe andika katika karatasi kuliko kujaribu kueleza watu unaweza usieleweke. Ni maneno mengi ambayo kwa kweli ningeweza kushauri lakini tuanzie na haya machache  kwanza.

NAFASI YA KAZI---ANAHITAJIKA MGANGA WA TIMU YETU

TANGAZO TANGAZO TANGAZO
Timu yetu ya soka sasa ina mwaka mmoja, lakini katika kipindi hiki tumekuwa tunafungwa karibu na kila timu, kamati kuu ya timu imegundua kuwa timu yetu inalogwa sana ndio maana tunafungwa, kwa hiyo uongozi umeamua kutangaza nafasi ya Mtaalamu Mkazi wa Timu.
Kazi ambazo Mtaalamu atalazimika kufanya ni zifuatazo;
- Kusafisha nyota ya timu ili tuweze kupata wafadhili
- kusafisha nyota za wachezaji ili wajulikane kimataifa
- kuhakikisha kila timu ikicheza inashinda
- kuvunja timu pinzani zisambaratike kabisa
-kuulinda uongozi ulioko madarakani na husda za watu wanaotaka kuupindua
Ili kupata mtaalam aliyebobea kutakua na usaili ambao utafanywa mwisho wa mwezi huu mbele ya viongozi wa timu. Mtaalamu anaeona anaweza kufanya kazi hii atume mamombi ili aelekezwe wapi aje kusailiwa.
KLABU YETU HOYEEEEEEEEEEEEEEEEE

18 September 2012

LEO NIMEKUMBUKA ENZI ZILEEEEEE

Nimekumbuka enzi ziiile ambazo Pikipiki ilikuwa haijaitwa Bodaboda, na Vigogo walikuwa wanaitwa Manaizi, hii ilikuwa kabla hawajaitwa Mabwanyenye. Kwanza niseme, waliitwa Manaizi kutokana na sera iliyojulikana kama Africanization, yaani mara tu baada ya Uhuru kulikuweko na kazi ya kuwaweka Waafrika katika vyeo vilivyokuwa vinashikiliwa na wazungu. Hawa Manaizi ndio walikuwa wenzetu ambao tulisota wote kudai Uhuru wao walipopata nafasi zilizokuwa za wazungu wakawa wengine kabisa wakaitwa Manaizi, kama leo jamaa mnasaidiana kudai haki, mnamchagua awe kiongozi wenu anageuka mtawala wenu halafu anakuwa Kigogo. Turudi kwenye mada, nakumbuka enzi zileee kabla warembo hawajaitwa, kichuna, kisura, kipusa, baadae kuitwa Kishtobe (kutokana na meli yenye jina hilo) , siku hizi dah, demu, gashi, changu, haya tena. Nakumbuka enzi zileee wakati kabla ya RTC, wakati kulikuweko na COSATA, hii ilikuwa kabla ya kuweko kwa BADEKO, MODECO, IDECO,MBEDEKO,BUDEKO, na kiukweli nakumbuka kabla ya kuweko maduka ya kaya, ambapo mwenye duka alikuwa na daftari inayoonyesha umenunua sukari kilo ngapi wiki hiyo, nakumbuka sana ule mwezi wa Februari 77, ambapo bia ya Safari ilianza kusambazwa , tukaanza kusikia watu wanapoteza fahamu kwa kunywa safari 3 tu, hiyo ilikuwa kabla wamama hawajawa na ujasiri wa kunywa Konyagi hadharani, hii ilikuja baada ya Konyagi chupa ndogo kuwa na bei ya shilingi 6 na nusu, ndio shilingi sita na senti hamsini, wakati Konyagi kubwa ilikuwa shilingi kumi na tatu. Guiness for power ilikuwa kinywaji cha kawaida, kule Iringa ilikuwa unanunua ulanzi lita tano  unachanganya na chupa moja ya guiness. Nakumbuka enzi zile za Pwagu na Pwaguzi hiyo ilikuwa baada ya kipindi maarufu cha Mahokaaaaaaaa eeee mama mbavu zanguuu. Nakumbuka enzi zileee wakati kulikuwa na gazeti la Ngurumo, Nyota, kiongozi, Mwenge, Reporter, na hiyo ilikuwa kabla gazeti la Baraza halijapigwa marufuku kutokana na kuandika vituko vya Manaizi kufumaniwa katika ukurasa wake wa pili uliojulikana kama Panapofuka Moshi, mwandishi wake akiwa FJ Khamis. Hiyo haikupishana sana na kufungiwa kwa gazeti la Reporter baada ya kutoa kibonzo kilichoonyesha Mwalimu kapakatwa na Mao Tse Tung wakati Mzee Kenyatta akikimbia mbio. Nakumbuka enzi zileee wakati Wamarekani walikuwa wanadondosha chakula kwa ndege kwenye sehemu zilizokuwa na njaa nchini, na nchi nzima kukaenea mafuta ya kupikia ya msaada, unga wa ugali wa njano, na buluga. Wakati huo Mzee makongoro akiimba Kuleni kuku mayai mboga samaki maziwa. Nakumbuka wakati ambapo RTD walikuwa wakitangaza 'live' dhifa za kitaifa na hapo wakati una njaa hujui utakula wapi unasikia mtangazaji akisema,' Na sasa namuona Waziri Mkuu amepakuwa wali uliopikwa kwa taaluma ya Kichina akiongeza na vipande vya miguu ya kuku iliyokaangwa vizuri na kujazia na sosi ya matunda  ambayo yameagizwa toka Uingereza anaenda pale kukaa na kula chakula kile' Nakumbuka  oh Nakumbuka 

17 September 2012

KWANINI BWANA HARUSI ANAVAA SUTI NYEUSI

Mtoto na mama yake kwenye harusi;
MTOTO: Mama kwanini bibi harusi anavaa nguo nyeupe?
MAMA: Nyeupe ni rangi ya furaha kwa hiyo bibi harusi anavaa nguo ile maana yake leo ndio siku yake ya kwanza ya kuanza kuishi maisha ya furaha tele
MTOTO: Sasa bwana harusi kwanini kavaa suti nyeusi?

UZEE HUO

JAMAA: Dokta sijisikii vizuri yaani nikiwa natembea macho yanaanza kuona vidotidoti
DOKTA: Uzee huo
JAMAA: Pia huwa nikiamka asubuhi mgongo unauma sana
DOKTA: Uzee huo
JAMAA: Kichwa pia huwa kinaniuma sana wakati wa mchana
DOKTA: Uzee huo
JAMAA: We dokta vipi kila ninalokwambia unanambia uzee huo, kama huwezi kunitibu nambie niende kutafuta matibabu kwingine
DOKTA: Unaona unavyowahi kukasirika ni wazi uzee huo

VUA MZEE UMEZIGEUZA

Mtu na mkewe walienda kwa mganga wa kienyeji, walikuwa na tatizo,  mume alikuwa goigoi kitandani. Mganga akawambia ana kanda mbili ambazo ukizivaa mara moja unakuwa na nguvu za ajabu katika mambo husika. Mume akaona huyu mganga feki;
MUME: Oyaa mke wangu twende huu ni ujinga, kanda mbili na matatizo yangu wapi kwa wapi?
MKE: Jamani si ungejaribu jamani, unadharau kitu hata hujui itakuwaje
MUME: Hebu tuondoke, waganga waongo lakini huyu ndio bingwa wao.
MGANGA: Si ungejaribu mzee, halafu ndio unilaani
MUME:(Kwa hasira) Haya leta......akavivaa, ghafla akapiga ukelele na kuvua nguo zake, na kuanza kumng'ang'ania mganga, mganga akawa anajitahidi kujinasua jasho linamtoka
MGANGA: Umegeuza,umegeuza kanda mbili, vua upesi umezigeuza ohhhhhh nisaidieni jamani

15 September 2012

MKEO YUKO NA RAFIKI YAKO

SAM: Aise Dula mkeo yuko Wakuja Gesti na rafiki yako, kimbia upesi uwawahi.....Haraka sana Dula kaacha shughuli zote na kukimbilia gesti. Dakika kumi baadae akarudi na hasira;
DULA: Hivi we Sam mbona muongo hivi, yule jamaa wala sio rafiki yangu, nimeumbuka kumsumbua mtu wa watu bure shauri yako wewe. Siku nyingine angalia vizuri

WADADA NIWAPE SIRI

WADADA NIWAPE SIRI, UKISIKIA MWANAUME ANASEMA;
Nakuchukulia kama dada yangu ana maana una sura mbaya
Sikupendi kimapenzi (una sura mbaya)
Sitaki kujihusisha na mapenzi kwa wakati huu (una sura mbaya)
Kiukweli nina girlfriend yuko masomoni (una sura mbaya)
Nakwepa kuwa na mahusiano na mtu ninaefanya nae kazi (una sura mbaya)
Tatizo sio wewe ni mimi (Una sura mbaya)
Nimeamua kuwa bachela mpaka kifo (una sura mbaya)
Tuwe marafiki tu (Una sura mbaya)

YA LEOLEO KWENYE DALADALA

Leo kwenye daladala wadada wawili walikuwa wanagombea siti;
KONDA: Kuweni wastaarabu wakina dada, acheni ugomvi, haya mzee  zaidi ndie akae kwenye kiti..........wote wawili wamekataa kukaa

MALAIKA HAWASOMI TWITTER

Mkaka wa kidijitali alifariki alipofika peponi akaingia chumba cha kusailiwa;
MALAIKA: Karibu peponi bwana hebu tuambie duniani ulikuwa unafanya kitu gani cha maana
MKAKA: Jamani kwani hamkuwa mnasoma twitter? Mbona kila kitu nilikuwa naandika

14 September 2012

MUME WANGU NAOMBA SIMU YAKO

MKE: Naomba simu yako plz
MUME: Ahh okay ngoja niwashe nilikuwa nimezima,
... Delete video
Delete picture
Delete music
Delete inbox
Delete sent items
Delete
Delete
Delete
Delete
Delete
Delete
Delete 
Delete
Delete
Delete
Delete
Delete
Delete 
Delete
Delete
FORMAT MeMoRY CARD
MUME: Hii hapa mke wangu sina cha kuficha
MKE: Jamani nilikuwa nataka tu kuangalia saa ngapi?

MKEO SIO MWAMINIFU

Boyfriend wa mke kaenda kwa mume;
BOYFRIEND: Aise kuna kitu kimeniudhi sana
MUME: Nini tena?
BOYFRIEND: Mkeo sio mwaminifu anatudanganya mimi na wewe

ALIFUMANIWA

Jamaa kaingia bar kamkuta kimwana mzuri, baada ya kupeana vinywaji vya kutosha;
MKAKA: Nimekupenda, unaonaje twende mahala faraga?
MDADA:Huna girlfriend?
MKAKA: Sina kabisaaaa, tuliachana siku nyingi.......masaa machache baadae wakati wanajitayarisha kutimka toka gesti;
MDADA: Mwanaume mzuri kama wewe inakuwaje ukaachana na  girlfriend wako?
MKAKA: Mke wangu alitufumania

CHEKA-PALE AKILI YA MWANAUME INAPO 'CEASE'

Mume akipoteza simu yake nyumbani ni mbaya anapata presha, ni mbaya zaidi akimuona mkewe kaiokota na ameishika mkononi, akili inasimama kufanya kazi

KANUNUE TIKETI WEWE

Jamaa mambo yalimuendea vibaya sana, biashara zilianguka, madeni yakamuandama, akawa ana sali sana, kila asubuhi akiamka anaanza,'EE Mungu nisaidie nishinde bahati nasibu niondokane na haya matatizo', akaendelea na sala hiyo, alipoona hakuna mabadiliko akabadili na sala,'E Mungu mbona unanitupa kiumbe wako, nimeomba unisaidie nishinde bahati nasibu'.
 Siku hiyo akawa amelala akaota malaika kamjia;
MALAIKA: Oyaa sala zako zimesikilizwa siku nyingi lakini kuna kitu nimetumwa kwako nikupe kwanza
JAMAA: Nini hicho?
MALAIKA: Nimetumwa nikutandike viboko sita kwanza.. Chap chap Malaika akamtandika viboko sita saaafi
MALAIKA: Hiyo adhabu yako ni fundisho, wewe unaomba ushinde bahati nasibu mwezi wa pili sasa lakini tiketi ya bahati nasibu hununui unadhani nani akununulie tiketi?

BAA HAIKO WAZI KWA KUWA IMEFUNGWA


NILIKUJARIBISHIA

Jamaa alipitia baa akautandika mtindi vizuri, kisha akapata kimwana wakaenda gesti. Kama saa tisa usiku kashtuka akavaa harakaharaka na kukimbilia kwake, mkewe mvumilivu akamfungulia mlango alipoingia akaanza uwongo kuwa alikamatwa na polisi ndio maana kachelewa, wakati huo akiwa anavua nguo, ghafla mke akagundua jamaa kavaa G string,
MKE: Mungu wangu, mume wangu we si uliondoka na boxer hapa?
MUME:(akiwa kachanganyikiwa sana) Er unajua nilikununulia hii chupi sasa nikaona nikujaribishie kabisa

13 September 2012

HIVI TULIKUTANA WAPI?

MKAKA:(Katika mbinu za kumzoea mdada) Samahani sister sijui nimewahi kukuona wapi?
MDADA: Uliniona hospitali ulipougua ugonjwa wa zinaa
MKAKA: Kavu sana wewe

12 September 2012

HAYA JAKI ANDIKA 55

MWALIMU: Haya Jaki andika 55
JAKI: Naandikaje?
MWALIMU: Andika 5 halafu pembeni yake andika 5 nyingine. Jaki akaandika 5 halafu akakwama kuendelea
MWALIMU: Tatizo gani tena jaki si umalizie
JAKI: Mwalimu hii 5 ingine niandike mbele au nyuma ya hii 5 ya kwanza?

MASIKIO YAMEZIBA MKOJO HAUTOKI

Jamaa kaingia chumba cha kumngojea daktari, akakaa anangojea zamu yake, ghafla akaingia mama mmoja na kukaa karibu na jamaa;
MMAMA: Mambo?
JAMAA: Poa
MMAMA: Unaumwa nini?
JAMAA: Sehemu za siri zimeziba....haraka sana yule mama akahama na kiti. Dakika chache baadae kakaingia kabibi nako kakaa karibu na jamaa kakauliza swali lilelile kakapewa majibu yaleyale, kumbe dokta alikuwa anasikia akatoka chumbani kwake;
DOKTA: Mheshimiwa sio vizuri kujibu direct namna hiyo maswali unatisha watu, si udanganye japo useme unaumwa sikio au pua.
JAMAA: Samahani dokta, huwa sipendi uwongo, lakini nimekuelewa.....muda si mrefu kaingia polisi mmoja akakaa karibu na jamaa na kuanza mazungumzo;
POLISI: Mwenzangu unaumwa nini?
JAMAA: Masikio
POLISI: Pole sana masikio bwana yanauma sana 
JAMAA: Yangu hayaumi ila yameziba mkojo hautoki

TUMEMZIKA MWAKA WA TATU SASA

MGENI: Hodii
MAMA: Karibu
MGENI: Mzee yupo?
MAMA: Hayupo
MGENI: Naweza kumsubiri?
MAMA: Ukiweza......baada ya kusubiri masaa matatu
MGENI: Kwani yuko wapi?
MAMA: Makaburini
MGENI: Kwani atarudi saa ngapi?
MAMA: Sijui, tumemzika mwaka wa tatu sasa

NIMEUA NYUKI NA iPAD

Juzi nimemtuma mpwa wangu anipe gazeti, kwanza kanicheka sana;
MPWA: Babu hatutumii magazeti siku hizi hebu chukua hii iPad yangu.. Ni kweli ilifaa sana maana nilimbamiza yule nyuki aliyekuwa ananisumbua akasagika kabisa, nashangaa mpwa wangu nimemrudishia iPad yake lakini hataki kuongea na mimi mpaka leo.

11 September 2012

NIMEJIUMA ULIMI NTAKUFA

Vinyoka vidogo viwili vilikuwa ninacheza;
KINYOKA 1: Eti sisi tuna sumu
KINYOKA 2: Ndio kwani vipi?
KINYOKA 1: Basi mi ntakufa
KINYOKA 2: Mbona sikuelewi
KINYOKA 1: Mwenzio nimejiuma ulimi

HAYA NENDA KWENU

MUME: Mke wangu je nikishinda bahati nasibu utafanya nini?
MKE: NtaCHUKUA nusu kisha ntakuacha
MUME: Safi sana nimecheza bahati nasibu nimeshinda shilingi alfu ishirini. Kumi yako hii hapa, na wewe sepa nenda kwenu.

GULO ANA MAKSI D

Jamaa alikuwa kaunta ya baa anateremsha kinywaji chake taratibu huku anasoma gazeti lile bingwa la kupindisha habari. Mara akaguswa bega;
MGUSABEGA: Samahani mzee unamfahamu Gulo Mweusi?...jamaa akatoa kanoti buku kake akaperuzi,
JAMAA: Gulo, Gulooo  eee G- G- G huyu hapa ndio namfahamu
MGUSABEGA: Mzee umewahi kulala nae?
JAMAA: Ndio
MGUSABEGA: Samahani mzee mimi ni mumewe na sijafurahishwa kabisa na kitendo hicho
JAMAA:(akaangalia tena kanoti buku) Hebu tuone Gulooo, D-D-D. Yap naona hapa hata mimi sikufurahishwa kabisaaa

AFRICA HAS GOT TALENT


FISADI MTAKATIFU

Kuna ndugu wawili ambao kiukweli walikuwa mafisadi wa hali ya juu, lakini walitumia utajiri wao huo kuficha ubaya wao, na wakawa wahudhuriaji wazuri wa kanisa ili waonekane ni watu wema. Bahati mbaya mchungaji wao ambaye alikuwa akiliongoza kanisa lile kwa muda mrefu akafariki akaja mchungaji mpya ambaye pamoja na kuwagundua mapema kuwa wale ndugu ni wanafiki, akaanza kuliendesha kanisa vizuri kiasi cha watu kuanza kuongezeka, hivyo ikalazimika kuanzisha harambee ya mchango kwa ajili ya kupanua kanisa. Mmoja wa wale ndugu akafariki wakati ule, mwenzake akamuendea mchungaji;
FISADI: Mchungaji, hapa nina cheki ambayo italipa gharama zote za ujenzi wa kanisa, lakini siku ya kumzika ndugu yangu italazimu umtangaze kuwa alikuwa ni mtu MTAKATIFU.........Mchungaji akapokea cheki kwa shukrani nyingi na haraka sana kuipeleka benki. Siku ya mazishi taratibu zote zikafuatwa hatimae mchungaji akaanza kutoa mahubiri
MCHUNGAJI:Hakuna siri kuwa marehemu alikuwa anaendesha genge la majambazi, alikuwa mwizi wa mali za umma , dhulumati, alikuwa muasherati mkubwa,mshirikina, ameharibu mabinti wetu wengi kwa fedha zake, alitumia rushwa kwa kufanikisha mambo yake, wote tunajua hakuwa mwaminifu kwa ndoa yake na mengine mengi. Lakini niwe mkweli, huyu bwana alikuwa MTAKATIFU ukilinganisha nandugu yake ambaye bado yuko hai.

KICHWA KITUPU

DOGO: mama tumbo linauma
MAMA: litakuwa tupu hilo, ngoja nikutengenezee uji.....Kesho yake;
MAMA: Mhh kichwa kinaniuma
DOGO: Kitakuwa kitupu icho

KUFUNGA IWE PIA INA HUSU KUTOTUMIA FACEBOOK

Kutokana na maendeleo ya teknolojia itafikia kwamba kufunga ni pamoja na kutotumia Facebook, Twitter na Blackberry. Nahisi kuna watu watakuwa makobe

WANAZUONI HEBU TUSAIDIANE (blackberry theorem)

BINADAMU=kula+kazi+blackberry+kulala
PUNDA=kula+kazi+kulala
kwa hiyo BINADAMU= Blackberry + Punda
au BINADAMU-Blackberry=Punda

DEMU WA FACEBOOK

MKAKA: Mpenzi tabu yako we una wivu sana
MDADA: Aka mi sina wivu hata kidogo
MKAKA: Una wivu bwana
MDADA: Nimejifunza mwanamke mwenye wivu hujiharibia mwenyewe
MKAKA: Nibusu basi
MDADA: Nenda kambusu demu wako uliye m'like' kwenye facebook

NAKUMBUKA NILIPOKUWA MWANAUME

Mbongo kaenda Thailand, katika zunguka yake akapata mpenzi wakaenda hotelini kwake na kulala mpaka asubuhi. Asubuhi yake mdada wa KiThai akawa anaonekana hana furaha;
MBONGO: Vipi honey mbona unaonekana huna raha?
MTHAI: Nimekumbuka tu enzi kabla sijapata operesheni nilipokuwa mwanaume.

10 September 2012

MGAMBO FALA

Mlevi alikuwa anakojoa kando ya barabara, mgambo akamzukia;
MGAMBO: We acha kukojoa funga zipu haraka. Mlevi akafunga zipu haraka, mgambo akaondoka. Mlevi akaanza kucheka
JIRANI: Sasa unacheka nini?
MLEVI: Mi mtoto wa mjini bwana, yaani nimemdanganya mgambo hivihivi?
JIRANI: Umefanya nini?
MLEVI: Nimefunga zipu lakini nikaendelea kukojoa kisiri kwenye suruali mpaka nimemaliza, na yule fala wala hakutambua.

OLE WAKO UKOHOE

Jamaa alikuwa anakohoa kwa muda mrefu sana, kila dawa akipewa anatulia siku mbili kisha anaanza tena. Siku hiyo akaenda kwa daktari ambaye akamwambia atampa dawa itakayomaliza matatizo. Baada ya hapo dokta akampa dawa ya kuharisha;
JAMAA: Dokta mi nakohoa sasa unanipa dawa hii si kila nikikohoa ntakuwa najiharishia?
DOKTA: Haswa, sasa ole wako ukohoe

JAMANI VUMILIA I LOVE YOU MWAAAAAH

Jambazi sugu ambalo tayari lilikwisha kaa gerezani kwa zaidi ya miaka kumi na tano lilitoroka jela. Na usiku uleule likaingia kwenye nyumba moja na kumkuta mtu na mkewe, ambapo baada ya kuwafunga kamba na  kutishia kuwauwa walikuwa watulivu kabisa. Jambazi akamuendea yule mke akambusu kwenye shavu na kumuuliza kitu kwa siri mke kisha akaelekea chumbani kwao.
MUME: Mke wangu huyu ni jambazi sugu muuwaji anaweza kutuuwa, nimemuona alivyokubusu ni wazi kutokana na kukaa miaka mingi gerezani anataka mwanamke. Najua itakuuma na kukutia kichefuchefu, nakuomba uvumilie najua akimaliza ataondoka itakuwa siri yetu. I love you, piga moyo konde mke wangu.
MKE:Kiukweli kanibusu lakini alikuwa ananiambia amekaa jela muda mrefu hamu ya wanawake imeisha na amekuona anakutamani ameniuliza chumbani wapi ili akuone akupeleke. Najua itakuuma na kukutia kichefuchefu, nakuomba uvumilie najua akimaliza ataondoka itakuwa siri yetu. I love you, piga moyo konde mume wangu

NIMEPONDWA NA FRIJI

Baunsa wa night club alienda kutibiwa kutokana na maumivu makali baada ya kupata mshtuko wa mgongo;
DOKTA: Umeumiaje?
BAUNSA:Nilipoingia nyumbani kwangu leo asubuhi, nilipata hisia kuwa mke wangu ana mtu chumbani kwetu,nikaingia chumbani kikomandoo nikamkuta mke wangu peke yake,mara nikasikia mlango wa sebuleni umefunguliwa kwafujo, nilipochungulia dirishani nikamwona mtu anakimbia huku anavaa shati, nikachukua fridge nikamrushia nikiwa ghorofa ya tatu,hapo ndipo niliposhtua uti wa mgongo.....Alipomaliza tu kauli yake,akaingia mgonjwa
mwingine kaharibika kama kagongwa na gari.

DOKTA: Vipi ndugu,nini kimekusibu?
MGONJWA:Nilisahau kuweka alarm asubuhi nikachelewa kuamka kwenda kazini, kazi yenyewe ndio kwanza nimeanza baada ya kukaa jobless kwa muda mrefu, nikatoka kwangu spidi huku navaa nguo, mara nikapondwa na fridge kichwani.

MLEVI KAIBIWA DEMU 'LIVE'

Mlevi katoka bar mkononi kashika funguo ya gari kasimama mbele ya bar akaanza kulia, askari akaja;
ASKARI : Wewe vipi tena?
MLEVI: Wameniibia gari
ASKARI: Ulipaki wapi?
MLEVI: Si unaona hii funguo, huku mwisho ilikuwa imeingia kwenye gari....askari akamuona kuwa jamaa kalewa mno, na pia alikuwa hajafunga zipu mambo yote yako nje
ASKARI: Wewe unajua na zipu hujafunga.....mlevi akajiangalia kisha akapiga kelele
MLEVI: Haaaa washenzi wakubwa wameniibia na demu wangu

MKE WANGU ANAFANYA BIASHARA YA KITIMOTO

Jamaa alikuwa baa anakunywa, rafiki yake akaja wakawa katika mazungumzo;
RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
RAFIKI: Nini tena?
JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?
JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja nauliza, "Huyo nguruwe umeshamuondoa?' Yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka

PATIA HUYU 20 THOUSAND NDIYO WEWE NATOKA

Munakumbuka ile mutu ya Kenya iko na stuck ndani ya muke ya mutu ingine? Mi iko na ile vidio ya huyo mjamaa, alikuwa anataka kulipa two thousand lakini ile bwana ya yule bibi naclaim 20thousand, na bibi yake ye hataki tena

HE UMEWAHI KUONJA UBUYU WA 5GB?


9 September 2012

SINA CHENJI ONGEZA KIDOGO

Mwanakijiji kamfumania jamaa na mkewe, baada ya heka heka kali za kumlamba ngumi na vichwa kadhaa;
MGONI: Nisamehe ndugu yangu sirudii tena, niko tayari kukulipa fidia
MUME: Nilipe alfu tano
MGONI: Sawa mzee ila nina alfu kumi hapa sijui chenji kama unayo?
MUME: Sina chenji, nakuachia mke dakika tano tu zaidi, ongeza kidogo halafu hatudaiani.

NIMECHANGANYA FANTA NA CHAI

WAKUJA: Kile nini chenye rangi nzuri?
MWENYE DUKA: Inaitwa Thermos, ukiweka kitu moto kinabaki moto, na ukiweka kitu baridi kinabaki baridi
WAKUJA: Aise safi sana niuzie....... Wakuja akainunua na wiki inayofuata akaenda nayo kazini kwake
JUMA: Wakuja nini hicho?
WAKUJA: Hii inaitwa thermos, ukiweka humu kitu cha moto kinabaki cha moto na kitu cha baridi kinabaki cha baridi
JUMA: Sasa umeweka nini humo?
WAKUJA: Nimweka vikombe viwili vya chai na chupa moja ya fanta

TV YA RANGI

WAKUJA: Shkamoo mwenye duka
MWENYEDUKA: Marahaba karibu unataka nini.
WAKUJA: NImeambiwa unauza TV za rangi
MWENYEDUKA: Haswa hili duka kubwa bwana, kila kitu cha electronics kiko hapa
WAKUJA: Naomba TV ya rangi ya kijani

7 September 2012

TEMBO KAFA

Askari wa wanyama pori alikutwa na watalii analia;
MTALII: Mbona unalia
ASKARI: Tembo kafa
MTALII: He ndio unalia hivi? Inaonekana unapenda sana wanyama
ASKARI: Hapana wamenipa kazi ya kumchimbia kaburi na kumzika

JINI LIKAMGEUZA AKAWA BLACKBERRY

Jamaa alikuwa anapita kando ya bahari akaokota chupa alipoifungua likatoka jini;
JINI: Loh asante sana nilifungiwa kwenye chupa hii miaka mia tisa iliyopita, asante sana kwa kuniweka huru, omba vitu viwili vyovyote mi ntakupa.
JAMAA: Kwanza nataka kuwa bilionea...hapo hapo jini likampa karatasi imeandikwa namba ya akaunti yenye mabilioni ya dola
JAMAA :Pili nataka kuwa kitu ambacho mabinti wanahamu nacho sana...jini likamgeuza akawa  Blackberry

SIMBA KATELEZA

MTANGANYIKA:Leo nimeponea chupuchupu kuuwawa na simba
MBONGO: He ilikuwaje?
MTANGANYIKA: Nilikuwa nimechuchumaa najisaidia nyuma ya chaka simba akatokea ghafla
MBONGO: Sasa uliponaje?
TANGANYIKA: Nakwambia kama sio simba kuteleza teleza ningekuwa marehemu.
MBONGO: E bwanaee hapo ningekuwa mimi kwa vyovyote ningejiharishia hovyo
TANGANYIKA: He kwani mimi nilifanya nini? Unafikiri simba alikuwa anateleza kwanini? We acha bwana simba anatisha bwana

WAONYESHE KIBALI MZEE

Bwana Miti alikwenda kutembelea kijiji kimoja kukagua utunzaji wa msitu uliokuuwa karibu na kijiji hicho. Akafika kwa Mwenyekiti wa Kijiji na kwa maringo sana akajitambulisha;
BWANAMITI: Mwenyekiti mi ndie Bwana Miti wa wilaya nimekuja kukagua kijiji chako maana nyie viongozi wa ngazi za chini mnatabia ya kukiuka taratibu
MWENYEKITI: Bwana mdogo nimezaliwa hapa ntakiukaje mambo ambayo yanaweza kuniletea hasara mwenyewe?
BWANAMITI; Ndio maneno yenu, haya mie naingia msituni kuona kama mmekata miti
MWENYEKITI: Sidhani kama ni muda mzuri wa kuingia katika pori hilo saa hizi.
BWANAMITI: Mwenyekiti mimi ni Bwanamiti wa Wilaya nina kibali cha kuingia msitu wowote katika wilaya hii wakati wowote ninaotaka
MWENYEKITI: Haya bwana mkubwa....Bwanamiti aliingia msituni lakini dakika chache baadae alitokea msituni akiwa katika mbio kali kitambi kikiwa kimewahi mbele;
BWANAMITI: Nyuki, nyuki mwenyekiti nyuki nakufaaa
MWENYEKITI: Waonyeshe kibali watakuachia

6 September 2012

NTAMTUNZIA ATAKAENIOA

MKAKA: I love you my baby
MDADA: Hata mimi lakini tupendane tu, mambo ya ngono staki, namtunzia mume atakaenioa
MKAKA: Hilo sio tatizo, hata mimi tupendane tu, usiniombe pesa namtunzia mke ntakae muoa

SI MACHIZI WOTE WAKO HOSPITALI


USIPIGE KELELE NATAKA KUTAGA

Machizi watano walitoroka toka hospitali yao wakaenda kujificha kwenye banda la kuku. Haikuchukua muda mrefu walikamatwa maana walikutwa wakirukaruka na kupiga kelele wakijifanya kuku ili wasionekane. Ila moja alikuwa kachuchumaa kimya, hivyo madaktari walipowakama wenzie yeye hawakumgusa maana walihisi japokuwa yeye ana unafuu.
DOKTA: Naona wewe umejirudi, siyo kama wenzio waliokuwa wanadhani wao kuku
MGONJWA: Shhhhhh usipige kelele nataka kutaga

BABA YAKE NI WEWE

TAJIRI: Namshukuru Mungu, kwa sasa nina magari mengi tu ya kifahari , nyumba kadhaa, mashamba na pesa nyingi benki, I am okay
MASIKINI: Mimi sina mali lakini nina mtoto mvulana ambaye kamjaza mimba binti mmoja, binti huyo ni mtoto pekee kwa babake. Babake nasikia ni wewe

KWA WASOMI TUUU

TAFSIRI KWA KIINGLEZA-BABA MIMI MTOTO WAKO WA NGAPI?

BREAKING NEEEWSSS-DUKA LA UBONGO-MNUNULIE MPENZI WAKO UBONGO MPYAAAAA

Je boifrend wako unampenda lakini hamnazo? Au Gelofrend wako unampenda lakini zuzu? Je mwanao ameshindwa kabisa kukariri 1+1? Je mumeo mapepe haeleweki? Au mkeo anashindwa kujifunza kingleza rahisi? Matatizo yote haya yamekwisha. Mnunulie ubongo mpya kabisa. Mali mpya zimefika wahi sasa umsapraiz mtu kwa kumpa zawadi ya new 'BRAINS'.

5 September 2012

HE UNAUGONJWA WA ZINAA?

Manesi wengine noma, jamaa alikuwa na appointment na dokta. Akamuendea nesi aliyekuwa akipokea wageni ambao walikuwa wengi wamejazana kwenye mabenchi wanasubiri huduma;
JAMAA: Samahani naomba kumuona dokta anishauri dawa vipimo hivi hapa...akampa nesi karatasi, nesi akasoma kile kikaratasi
NESI: ( Kwa sauti kubwa) He kumbe una ugonjwa wa zinaa
JAMAA: (Nae kwa sauti) Ndio, dokta alinambia na wewe ulikusumbua kwa muda mrefu sana

TALAKA YA NINI? SUBIRI

Jamaa kamfumania mkewe;
JAMAA: Yaani mke wangu unanifanyia hivi mimi? Kitu gani nimekukosea?
MKE: Mume wangu najisikia aibu kubwa sana, nimekutendea kitu kibaya sana, naomba unipe talaka upate mtu mwaminifu
JAMAA: Ngoja kwanza mbona umefika mbali sana? Kosa lenyewe ni la kwanza talaka ya nini?

MASUPASTA WATAFUTA PA KUJICHIMBIA

Masupasta wawili maarufu walikuwa wanazunguka kwenye maduka mjini wakiingia kila duka na kuonyesha vimbwanga kuwa wao ni masupasta. Wakaingia duka moja wakaangalia nguo zilizotundikwa kwenye henga, hatimae wakaanza kuzijaribu kwa mbwembwe, na kuwafukuza wahudumu wote waliotaka kuwashauri, japo tayari watu walianza kukusanyika wakiwashangaa, wao wakaona huo ndio ujiko wenyewe. Hatimae mwenye duka akaja,' Samahani tunawaomba muache kujaribu nguo za watu, Je, mnajua kuwa hapa ni Dry Cleaner siyo duka la nguo'

BREAKING NEWSSSSS-KUNA MUONGO HUKU CLUB JAMANI

Wadada wengine waongo, yaani mpaka nimeamua kuondoka hapa club kwa ajili yake. Kawakusanya wenzie anawahadithia kuhusu mambo mbalimbali ya duniani. Eti Marekani jua huwa halitui, Aliwahi kufanya kazi ya kuwauzia Ice cream Waeskimo, tisa kumi nimeondoka alipowaambia watoto wa watu eti akiwa anasafiri na ndege  kwenda Ulaya huwa anapenda kukaa siti za dirishani, maana inakuwa rahisi joto likizidi kufungua dirisha kupunga upepo

'MI SIVAAGI CHUPI BABA SHAHIDI"

MMAMA: Huyo mtoto kanishinda namrudisha kijijini
MBABA: Vipi tena kwani kafanya nini?
MMAMA: Mwizi, kaniibia chupi zangu
MBABA: We unasikia mamako anachosema, umemuibia nguo zake?
HAUSGELO: Baba mi mama ananionea niibie chupi za nini? wewe mwenyewe shahidi yangu mi huwa sivaagi chupi......kesi mpya ikaanza

I AM FULL MAN, I WANT TO MERRY


Dear Lads and gentlemens of Facbook, goodmoning. I am now full man, I want to merry. My Father and my mother they I am saying get marryd. I am see meny gelz and wimens in the facbook, it is say still single. I am is very good face, smilling face, I am also in Kiswahili langwej mtanashati. My father has richness of many cows for cow milk, if you come you will get many milk.  I am studied education of o levo.in St Jon seco, english medium, of internatshno teachers of Uganda and Kenya East Africa. Teacher is teaching many things to us, if you come you will enjoy. I have TV and gas cooker of 3 plates, I have sofa set ‘magongo’. I am working in Indian house, I am get very very expensive salary, if you come you will enjoy. Please beautiful gelz and wimens of facbook I love you very very, so say yes for me to merry you you will enjoy.