PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Walimu acheni kumnyanyasa mwanangu


Mama mmoja kenda kumtembelea mwanae shuleni, akakuta darasa la mwanae wako nje wanacheza. Bahati mbaya akamkuta mwanae kasimama peke yake wakati wenzie wanacheza kwa furaha. Akakaa kama dakika tano akaona mwanae kasimama mahala pamoja hatoki wala haendi kujiunga na wenzie;
MMAMA: Mwalimu kwanini mtoto wangu unambagua?
MWALIMU: Kwani vipi mama?
MMAMA: Usijifanye hujui, nimekaa hapa kitambo, namwona mwanangu mmemtenga wakati wenzie wanacheza wanafurahi.
MWALIMU: Mbona sikuelewi mama?
MMAMA: Hunielewi nini? Mnajidai mara mnagoma mara nini kumbe kazi kutesa watoto wa wenzenu, hebu muangalie mtoto wenzie wanacheza na mpira yeye mmemsimamisha tu pale kaganda
MWALIMU: Mama mwanao golikipa, ndio mana kasimama peke yake

Comments

Anonymous said…
VICHEKESHO VYAKO VINA VIWANGO VYA TBS
JFK said…
Hahahahaha asante mkuu