PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

WABABA VS WAMAMA

Kuna tofauti kubwa kati ya utoaji wa habari wa wababa na wamama. Kwa mfano;
MBABA: Aise unamumbuka yule jamaa mnene aliyekuwa anafanya fujo kwenye harusi ya mdogo wako? Basi kafa jana. Lakini habari hiyo ikiletwa na wamama inakuwa hivi;
MMAMA: Unamkumbuka yule rafiki yangu Lusi, basi kanipigia simu kasema Mama Vero kasikia kutoka kwa dadake Bupe kuwa yule Jamaa mnene aliyepelekwa polisi baada ya kufanya fujo wakati wa kutoa zawadi kwenye harusi ya Tina, juzi alikabwa na mfupa kooni wakati anakula kitimoto kwenye baa moja Kimara Mbezi, basi watu wakahangaika wakambeba mpaka barabarani, yaani unaambiwa Watanzania walivyo na roho mbaya magari yalikuwa yanapita tu kila wakijaribu kusimamamisha, hatimae wakapata kibajaji wakamkimbiza mpaka kadispensari kajirani kule wakakuta dokta kalewa njwii mikonyagi yake, wakaamua kumpeleka Muhimbili. Wamefika kule kumbe jamaa ameshajifia zamani.

Comments