PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Vaa upesi kaite ambulensi


Jamaa karudi ghafla nyumbani si akasikia sauti za ajabu toka chumbani kwake, akapiga ukelele na kuvunja mlango akamkuta mkewe akitetemeka;
Jamaa: We vipi?
Mke: Presha imepanda, jamaa akakimbia sebuleni ili apige simu ambulensi ije wakati anahangaika kutafuta namba, mwanae akaja akamwabia,'Baba anko yuko uchi kwenye kabati chumbani', jamaa akatupa simu na kurudi chumbani alipofungua mlango wa kabati akamkuta mdogo wake kabatini bile nguo nae anatetemeka ,
Jamaa: Na wewe vipi unazubaazubaa bila nguo wakati mke wangu ameshikwa na presha. Vaa upesi kaite ambulance

Comments