PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Tatizo mke wangu hajafa


Ajali mbaya ilitokea, akina mama ambao wote ni wake za watu waliamua kwenda kutalii mbuga za wanyama,wakati wanaenda huko basi lao likatumbukia mtoni akina mama wote wakafariki. Zilifuata wiki mbili za majonzi makubwa na baada ya hapo watu wakaanza kusahau, lakini Deus akawa kila akiingia bar baada ya bia mbili anaanza kulia;
DEUS: Mke wangu eeee kwanini lakini? kwanii jamani? Watu walimpa pole lakini akawa hanyamazi,mwisho jamaa mmoja akaona amuondolee uvivu.
Jamaa: Aise umezidi sasa, kama kufiwa wanaume wengi wamefiwa na wamekwisha nyamaza kwani mkeo alikuwa na nini zaidi?
DEUS: (Huku akilia),Nyinyi hamjui yaliyonikuta, mimi mke wangu alichelewa lile basi.Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Comments