HATUPIMI BANDO

2 August 2012

TANGAZO LA KUSUDIO LA KUGOMA

TANGAZO LA KUSUDIO LA KUGOMA:
Sisi watoto tulio na umri chini ya miaka mitatu tunakusudia kugoma ili kupata haki yetu ambayo tumeporwa na watu wasio na utu wala huruma. Inaeleweka wazi kuwa sisi ndie wenye haki ya jina la BABY. Kwa ufisadi wa hali ya juu jina letu limeporwa ambapo sasa vigogo, Mawaziri, Wabunge tena wa kambi zote, wazee sana, wazee wa kati, mapedeshe na masharobaro, mayanki na mafisadi wa jina hili wote eti nao wanaitwa BABY, hii si sawa kabisa. Tunaipa serikali siku saba kupiga marufuku matumizi ya jina hili kwa wasiohusika kinyume cha hapo, patachimbika, tutaanza kwa mgomo usio na kikomo nchi nzima na hatimae kuona namna ya kuweza kuunganisha nguvu na BABY wenzetu halali dunia nzima.
HILI NI ONYO LA MWISHO

1 comment:

Jiang said...

ha haaa...mi naiiba hii to www.mamanamwana.blogspot.com