PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

TANGAZO KUHUSU SABUNI ZA GESTI

TANGAZO TANGAZO TANGAZO
Nyie wenye magesti, kwa sababu ambazo ngumu kuzielewa mmeamua wote muwe mnawawekea wateja visabuni fulani vyenye harufu ambayo ni ya kipekee kabisa vyumbani mwao, hivyo ukitumia visabuni hivyo, hata ukiingia kwenye daladala wadau wanajua umetoka kuoga gesti. Hili ni jambo linakwaza sana maana utaona watu wanakuangalia kwa jicho la kukuhukumu kuwa umetoka kufanya mambo yasiyokubalika, kumbe maskini we ni mgeni umetoka kulala nyumba ya wageni. Baada ya kupata taarifa kuhusu hili ningependa kuwashauri watumiaji wa gesti kuanza kutembea na sabuni zao zenye harufu ambayo wameizoea au la kuoga bila kutumia sabuni za gesti ili kulinda heshima yao, nawasilisha hoja

Comments