PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

SIRI KUBWA YA KUONYESHA UMAHIRI KATIKA KAMATI


Siri kubwa ya kuonekana unafaa katika kamati:-
- kamwe usiwahi katika mkutano ni dalili ya kuwa we si mzoefu wa vikao
- Usiongee kitu mpaka mkutano japo umeshafikia nusu, hili litakufanya uonekane una busara ya kusikiliza kwa makini kinachoendelea kabla ya kutoa uamuzi
- Unapoongea kitu, hakikisha hakieleweki sawasawa hii itakufanya usiwe na ugomvi na mtu yoyote
- Ukiona kuna swala gumu na huna jibu, anzisha hoja ya kutengenezwa kwa kamati ndogo ya kushughulikia tatizo hilo
- Uwe mtu wa kwanza wa kutoa hoja ya kuahirisha kikao. Hii itakufanya upendwe na kila mtu maana wanakamati wote hutaka kikao kiishe lakini wanaogopa kusema

Comments