PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Siku nilipopata NOAH mpya ya bureeee


Dah mambo mengine bwana, juzi nilipita pale Sinza darajani nikielekea home nikaona mfuko umetupwa, kuuangalia ndani nimekuta dola 20,000. Niwe mkweli woga ulinishika nikaangalia kushoto na kulia nilipoona watu hawanioni nikachukua ule mfuko na kwenda haraka home. Nilipomwaga kila kitu nikakuta vitambulisho, kadi za ATM, makaratasi mengi na iphone, nilitaka kuzima simu nitoe sim kadi lakini nikaacha roho ikanisuta kuwa mwenye mali anaweza akanipigia. Na kweli baada ya muda si mrefu simu ililia na kwa maelezo ikawa wazi mali zile ni za aliyepiga simu, nikamuelekeza niliko akaja kuchukua mzigo wake akanipa dola 2000 nikakataa kistaarabu, akachukua namba yangu akaondoka. Jana akanipigia simu kuwa yuko nje ya nyumba yangu alikuwa kaja na NOAH mpya kabisa, akanipa ufunguo na kuniambia hiyo ni zawadi yangu kutokana na tabia niliyoonyesha. Nikamshukuru sana wala sikuamini macho yangu, ile nataka kuwasha gari nilitest si nikasikia,'Baba baba amka chakula tayari'

Comments

Mdigo said…
Bwana Kitime shukran kaka kwa jitihada na blog hii yako ya burudani. Kaka ninazidi kukuombea mungu uendelee kuburudisha na kutuma vibwagizo vipya kila siku. Tulio nje ya nchi blog yako inatupa barudani ambayo haisemeki kwa kifupi nitatia neno la kiingereza "therapeutical creation". Nitamalizia kwa kutoa shukrani zangu za dhati na kila la kheri na blog.