HATUPIMI BANDO

15 August 2012

NYIE NENDENI TU


Dreva wa Bodaboda kapata abiria wawili, akawapakia mshkaki wakiwa njiani abiria wakaanza mazungumzo,
ABIRIA 1: Hivi kwenye pisto yako zimebaki risasi ngapi?
ABIRIA 2: Zimebaki 5
ABIRIA 1: Acha uhuni we unajua risasi bei mbaya, umepeleka wapi risasi moja?
ABIRIA 2: Si unakumbuka yule dereva wa bodaboda mbishi si ililazimika nimtwange risasi nyingine ya ziada...(wakati huu dereva wa bodaboda alikuwa anakaribiwa kuchafua suruali). Akawafikisha abiria wake walipotaka kufika, walipotaka kumpa nauli akawajibu huku akichekacheka
DEREVA: Msiwe na wasi wasi tunasaidiana, sisi wote ni Wabongo karibuni tena, nyie nendeni tu

No comments: