PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Nimefukia pesa Sinza Darajani


Jamaa alipandia daladala Sinza Darajani, akapata siti, akaanza kuchat kwenye simu na rafiki yake, si akagundua jamaa mmoja anasoma kila anchotuma. Basi bila kuonyesha dalili ya kuudhika akaandika, 'Aise zile pesa niliona nyingi mno polisi watanishtukia, hivyo nimezificha chini ya daraja pale Sinza darajani, nimefukia kwenye mfuko wa plastiki kwenye maji machafu kushoto kwenye nguzo ya daraja'. Jamaa aliyekuwa anakodoloea macho text si akashuka haraka kituo kilichofuata.

Comments