PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Nilibanwa nikaona ni heri niziume zile korodani


Vijiji  viwili vilikuwa vinashindana katika mieleka, wakabakia mabingwa wawili kupambana katika fainali Mwakimwagu na Mgano. Bingwa wa kijiji kimoja Mwakimwagu, ambaye kwa miaka minne mfululizo amekuwa anashinda, alionekana wazi atakuwa bingwa tena maana alikuwa na staili yake ya kibano iliyojulikana kwa wote kama ‘Shokolokobango’, akikubana na loki hiyo hutoki. Mwalimu wa Mgano akamuonya tena mwanafunzi wake kuwa hata iweje asikubali kutegwa akajikuta anabanwa na Shokolokobango. Mpambano ukaanza, mabingwa wakaanza kuzungukana na kupimana ubavu, pamoja na kukwepa kwingi ghafla Mwakimwagu akamuwahi Mgano na kumbana na Shokolokobango, watu wote wakajua pambano litaisha baada ya sekunde chache maana Mgano lazima ataomba suluhu. Ghafla ukasikika ukelele mmoja mkali, na hapo Mwakimwagu alirushwa juu kama mtoto na kuanguka kama gunia la mchanga, Mgano akawa ameshinda, na kumnyang’anya ubingwa Mwakimwagu licha ya staili yake ya kutisha ya Shokolokobango. Kila mtu akashangaa na hasa mwalimu wa Mgano, akaona muulize mwanafunzi wake aliwezaje kujitoa kwenye ile kabali maarufu. Mgano hakuwa mchoyo wa maelezo akasema,’
MGANO: Kwa kweli nilipobanwa tu niliona kama vile nakamuliwa kila kitu, macho yalikuwa kama yanataka kutoka, haja kubwa pia nilihisi inatoka, nikawa tayari kupiga kelele niachiwe, nilipofungua macho kwa mshangao nikaona korodani mbele ya macho yangu, nikaona hapahapa, nikanyoosha shingo na kufungua mdomo na kuzing’ata gololi zile kwa nguvu zote’
MWALIMU: Alaaa kumbe ndicho kilichommaliza?
MGANO: Hapana, bwana,kwa kweli hata mimi nilishangaa  nguvu nilizopata ghafla baada ya kujing’ata korodani zangu mwenyewe

Comments