PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Ngoja tukakuitie mbuzi wa Mzee Kitime...

Dreva kazimikiwa gari lake karibu na kijiji kimoja. Akiwa kainama anajaribu kuangalia sababu ya tatizo hilo, ng'ombe mmoja akapita karibu;
NG'OMBE: Pole mzee, jaribu kuangalia plag kama zinachoma, ikiwa sio hivyo, cheki fyuzi....Jamaa akashtuka sana kusikia ng'ombe akiongea, basi akatoka mbio kuelekea kwenye kijiji, njiani akiwa anahema akakutana na jamaa wawili;
DREVA: Jamani nimekutana na ng'ombe anaongea
MWANAKIJIJI 1: Kwani ilikuwaje?
DREVA: Gari langu limezimika wakati najaribu kutengeneza akaja ng'ombe akaanza kuongea, ananiambia niangalie plag
MWANAKIJIJI 2: Ng'ombe mwenyewe rangi gani?
DREVA: Mweusi ana madoa meupe.... Wanakijiji wakaanguka kicheko kwa pamoja
MWANAKIJIJI 1: Hahahahahahaha kumbe ni yule, aise ng'ombe muongo yule kijiji kizima, toka lini akajua kutengeneza gari? Ngoja tukakuitie mbuzi wa Mzee Kitime yule ndio anaujuzi wa magari....JAMAA AKAZIMIA 

Comments