PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Ndoa yangu shwaaariiii

JIRANI: Ndugu yangu mbona ndoa yako imetulia hakuna matatizo, mi kwangu ni kasheshe kila siku?
DEVI: Hakuna siri, tumegawana majukumu. Mke wangu anatoa maamuzi kuhusu mambo madogomadogo na mimi nashughulika na mambo mazitomazito.
JIRANI: Sijakupata
DEVI: Mambo kama vile tujenge wapi, mshara utatumika vipi, tuweke benki shilingi ngapi, tuwe na watoto wangapi haya ni mambo madogomadogo yanashughulikiwa na mke wangu, mimi kazi yangu ni kuyakubali tu.
JAMAA: Na makubwa ni yepi?
DEVI: Mambo makubwa ni kwa mfano je, tuingie vitani na Malawi? Marekani iipige Iran? Je tujiunge na muungano wa Afrika Mashariki?, Je tutumie njia gani kumaliza vita vya Syria? hayo ndio mambo ninayoshughulikia na hatuingiliani hivyo ndoa kwa kweli imekuwa na amani kubwa.

Comments