HATUPIMI BANDO

26 August 2012

MKE WANGU HANIAAMINI KABISA KWA HILI

Mfugaji mmoja kakutwa bar kalewa wakati kwa kawaida hanywi pombe.
RAFIKI:He vipi tena hata wewe leo umelewa
MFUGAJI: We acha bwana we acha, nimechanganyikiwa hapa
RAFIKI: Kuna nini nikusaidie?
MFUGAJI: Alfajiri niliamka ili nikammkamue ng'ombe maziwa. Leo ng'ombe kawa mkorofi sana hataki kukamuliwa ananitwanga mateke, nikatafuta kamba nikatanua miguu nikamfunga kwenye  nguzo, kisha nikaunyanyua mkia nikaufunga kwenye kenchi, nilipomaliza kazi hii nikaamua kukojoa kabla ya kuanza kumkamua, ile namaliza kukojoa si mke wangu kaingia.
MKE:Heee mume wangu unamfanya nini ng'ombe?
Nimejaribu kumueleza kuwa nilikuwa namtayarisha ng'ombe kumkamua haelewi kitu

No comments: