PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

MGANGA NISAIDIE NINA MATATIZO MAKUBWA

KIGOGO: Mganga nisaidie nina matatizo makubwa.
MGANGA: Tawile ongea 
KIGOGO: Nina mahekalu manne Masaki, moja Bunju, Mwanza manne, Dodoma moja, Kinondoni nyumba arobaini, mke wangu kenda likizo, kuwatembelea watoto wanaosoma Marikani. Mdogo wangu nimemfungulia vituo vitatu vya mafuta. Nina nyumba ndogo 5, kila moja nimemjengea nyumba yake na kumnunulia gari lake. Nina magari matano kila moja lenye thamani ya shilingi milioni mia mbili
MGANGA: Mungu wangu mbona raha tupu, sasa tatizo liko wapi?
KIGOGO: Mshahara wangu laki sita kwa mwezi, na Waziri kanishitukia kanisimamisha kazi

Comments