HATUPIMI BANDO

19 August 2012

Mama yuko juu ya paa

Jamaa mmoja alikuwa akiishi na mdogo wake na mama yake, pia wakawa na kambwa ambako jamaa alikapenda mno. Siku moja akapata safari ya wiki moja, siku aliporudi tu kabla hajaingia ndani, mdogo wake akamuwahi;
DOGO: Kaka mbwa wako kafariki juzi......jamaa alisikitika sana, na zaidi hakupenda jinsi alivyopewa taarifa ya msiba huu
MJAMAA: We vipi unaona nilivyoshtuka, ilitakiwa  jambo la msiba kama hili ungeanza kunambia, mbwa wako yuko juu ya paa, halafu unanambia mbwa kadondoka toka kwenye paa, nakuwa nimejitayarisha utakaponambia mbwa kafa sawa wewe?
DOGO: Sawa kaka ntajirekibisha
MJAMAA: Mama yuko wapi?
DOGO: Mama yuko juu ya paa
MJAMAA: Ehh!

No comments: