PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

KWA KUWA HUJUI JIBU NDO UNAKUWA MKALI HIVYO?


Siku hiyo simba aliamka na kisirani, akamkuta nyani kwa ukali sana akauliza,'Nani mfalme wa wanyama wote?', nyani akawahi,'Simba". Simba akakutana na ng'ombe,'Wewe nani mfalme wa wanyama wote?', Ng'ombe akajibu kwa upole,'Simba'. Hatimae simba akakutana na tembo, akamuuliza naye,'We Bigi nani mfalme wa wanyama wote?', Tembo akamkamata simba akambamiza kwenye mti kama mara tatu hivi kisha akamkanyaga simba akawa hoi, lakini kabla hajapoteza fahamu Simba akasema kwa unyonge,' Sasa ndugu yangu kwa kuwa hujui jibu ndio uwe mkali hivyo?'

Comments

shame wakitaa said…
anapenda ukubwa alaf analolote!