PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Kuzaliwa iwe kwa maafikiano yenye mpangomkakati unaoeleweka

Hapa kwetu kuna watu wengi wanaoshughulika na kutetea haki za binadamu, ni jambo zuri, lakini kuna jambo moja ambalo lazima lisemwe, kuna haki kubwa sana inakiukwa, nashangaa hakuna anayeitetea, hata mama mwenye mvi nae sijamuona akishikia bango haki hii, nayo ni haki ya huyu binadamu kuzaliwa. Kiukweli kuna haki hapa inakiukwa, haki ya kuchagua kuzaliwa au kutozaliwa. Nilitegemea waheshimiwa wanaharakati wangelishikia bango hili tatizo la kulazimishwa kuzaliwa bila kuwa na mazungumzo ya awali na mtu yoyote, hii inaletea watu kuzaliwa kwa wazazi ambao hawana mpango mkakati wowote kuhusu mzaliwa husika, na hii baadae kuleta  shida kubwa na hivyo muhusika bila kupenda anaishi maisha kwa shida sana. Umefika wakati wanaharakati kutengeneza taratibu za makubaliano ili wanaotaka kuzaa waafikiane na anayetegemea kuzaliwa kuwa kaafiki hao kuwa wazazi wake. Mtu uwe unajua mapema baba yako ananafasi ya kufisadi? au ni pedeshe, au ni mlevi wa kutupwa atakayekupa matatizo maisha yako yote. Hii itaambatana na kuchagua kabila na ukoo wa kuzaliwa, na hata jina la ukoo. Nawasilisha hoja

Comments