PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Kuna madereva wana ugonjwa wa kupiga honi

Utafiti niliofanya unaonyesha Dar kuna madereva wana ugonjwa unaitwa, Honiyasis. Dereva akikumbwa na virusi vya ugonjwa huu, hupiga honi kwa kila kitu.
Hupiga honi akisha washa tu gari, eti anacheki kama betri ina chaji
Hupiga honi wakati anaondoa gari
Hupiga honi akianza kurudi rivas
Hupiga honi akitaka kuovateki
Hupiga honi gari jingiune likimuovateki
Hupiga honi akitaka kukata kona
Hupiga honi akitaka kuingia barabara kubwa
Hupiga honi kusalimia maderreva wenzie
Hupiga honi kumsalimia baba yake, mama yake mmjomba wake na kadhalika
Hupiga honi akikasirika
Hupiga honi akifuatia muziki kwenye radio yake
Hupiga honi kumlazimisha trafiki asimamishe watu wengi ili yeye apite
Hupiga honi kabla ajali haijatokea
Hupiga honi akisikia wenzie wanapiga honi

Comments