HATUPIMI BANDO

8 August 2012

Kanajua ntakufa kesho


Mzee mmoja lakini mwenye pesa sana aliingia kwenye hoteli moja maarufu na msichana mzuri sana mdogomdogo, akakutana na rafiki yake chooni,
Rafiki: Aise naona leo umetujia na kisichana kidogoo
Babu: Mke wangu yule nimemuoa
Rafiki: Mkeo? kakubalije kuolewa na zee kama wewe?
Babu: Nimekadanganya umri wangu.
Rafiki: Hahahaha Umekaambia una miaka 50?
Babu: Aaaaa wapi nimekaambia nina miaka 98, wakati nina miaka 70. Kanaimani nitakufa karibuni
Babu na Rafiki: Hahahahahahaha teh teh teh teh wakatoka chooni na kurudi kwenye meza zao

No comments: